MAJUKUMU YA IDARA YA USAFI NA MAZINGIRA
I: HIFADHI YA MAZINGIRA
(i)Utunzaji/Uhifadhi wa Mazingira na Bionuani (Environmental Conservation and Biodiversity);
i.Kutenga maeneo ya Upandaji Miti, Majani, Maua, Ukatiaji Miti na Upendezeshaji Mazingira (Planting of Trees, Plants, Grass, Flowers, Pruning of Trees and Beautification) na kusimamia Kampeni ya Taifa ya upandaji miti;
iiKuhamasisha jamii kushiriki na kuratibu Upandaji Miti, Majani, Maua, Ukatiaji Miti na Upendezeshaji Mazingira (Planting of Trees, Plants, Grass, Flowers, Pruning of Trees and Beautification) pamoja na utekelezaji wa mashindano ya Tuzo ya Rais ya kuhifadhi vyanzo vya maji, kupanda na kutunza miti katika Halmashauri husika.
iii.Kuhamasisha jamii kupanda miti, majani na maua, kukatia majani na miti na kupendezesha Miji na maeneo mbalimbali.
iv.Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya Halmashauri ya usimamizi wa Mazingira kwa kuzingatia Mpango Kazi wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.
v.Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sheria na miongozo ya kulinda mazingira ikiwa ni pamoja na bianuani, ardhi, mazingira ya mito, maziwa, bahari na mabwawa;
vi.Kuweka mfumo wa kukusanya taarifa za mazingira utakao husisha ngazi ya Halmashauri hadi kitongoji/mtaa;
vii.Kubaini maeneo ya hatari yanayohitaji usimamizi maalumu na kumshauri Waziri mwenye dhamana ya Usimamizi wa Mazingira kuhusu njia bora zinazoweza kutumika;
viii.Kuandaa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya maeneo yao zitakazojumuishwa katika Ripoti ya Taifa ya Hali ya Mazingira.
ix.Kupendekeza maeneo yanayoweza kutangazwa kuwa maeneo ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira na kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya Usimamizi wa Mazingira ya Hifadhi;
x.Kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kudhibiti utekelezaji wa shughuli yoyote inayoweza kuleta athari katika maeneo mito, maziwa, bahari na mabwawa;
xi.Kusimamia na kutekeleza Sera ya Taifa ya Mazingira, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kuhusu masuala ya hifadhi ya bioanuai yaliyobainishwa katika Sera, Sheria, Kununi, Miongozo, Mikakati, Mipango na Programu za Kisekta; na
xii.Kutekeleza Mikakati, Mipango na Programu ya Mikataba ya Kimataifa na Kanda inayohusiana na hifadhi ya bioanuai;
xiii.Kuandaa na kutekeleza program za kutoa elimu kuhusu hifadhi endelevu ya bioanuai katika maeneo yao;
xiv.Kubaini bioanuai zilizopo katika Halmashauri zao na hali ya uharibifu na uhifadhi wake;
xv.Kuweka na kusimamia mikakati ya kuongoa ardhi iliyoharibiwa na kuzuia uharibifu wa bioanuai;
xvi.Kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya Halmashauri husika.
xvii.Kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango na program za Halmashauri kwa kuzingatia Mkakati wa Matumizi Salama ya Teknolojia ya Kisasa (biosnfety);
xviii.Kutekeleza mfumo wa upashanaji habari juu ya Bioanuai na matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa;
xix.Kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala pamoja na majiko banifu;
xx.Kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali kuhusu Usimamizi wa Hifadhi ya Mazingira;
xxi.Kutoa mapendekezo na kufuatilia hatua za kukabiliana na uharibifu wa maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizo endelevu (kama uchimbaji madini, kilimo, ujenzi, ufugaji n.k.) ;na
xxii.Kusimamia na kutekeleza kazi nyingine zitakazoelekezwa na Mamlaka za juu.
2. Udhibiti Uchafuzi wa Mazingira (Ardhi, Maji, Hewa na Sauti (Poliution Controk: Land, Water, Air and Sound)
i.Kuandaa na kutekeleza programu za kuto elimu ya mazingira kwa jamii kuhusu njia bora za kudhibiti uchafuzi wa mazingira na athari zake;
ii.Kuweka na kusimamia amri za kudhibiti/kuzuia kelele, mitetemo na uchafuzi wa hewa unaosababishwa na moshi, gesitaka au gesi za sumu, kutoka vyanzo mbalimbali kama vile makazi, viwanda, uchimbaji wa madini na vyombo vya usafiri;
iii.Kuweka miongozo ya kupunguza athari za uchafuzi wa hewa ya ndani ya makazi (in-door pollution) inayosababishwa na shughuli mbalimbali kama vile matumizi ya nishati ya kuni, vinyesi vya mifugo na uchomaji wa madini ya zebaki;
iv.Kuandaa na kusmamia miongozi ya kutenganisha maeneo ya makazi ya watu, ofisi na taasisi za elimu na shughuli za kiuchumi kama vile ujenzi wa viwanda, madampo ili kudhibiti athari kwa afya na mazingira;
v.Kuandaa miongozo ya ujenzi wa miundombinu ya taka katika maeneo ya biashara, viwanda na shughuli nyingine za kiuchumi naya usimamizi wake ili kuhakikisha hali ya usafi na kudhibiti viumbe waharibifu na uzagaaji wa taka;
vi.Kuweka na kusimamia miongozo ya usimamizi wa majitaka katika kiundombinu ya kuhifadhi, kusafirisha na kutibu majitaka kwa kushirikiana na Mamlaka husika;
vii.Kufuatilia uzingatiaji wa viwango vilivyowekwa vya majitaka yanyomwanga kwenye mazingira ili kukidhi Viwango vya Mazingira.
viii.Kusimamia uzingatiaji na utekelezaji wa viwango vya mazingira vya Taifa na kuweka vigezo vya kupima uharibifu wa mazingira;
ix.Kufuatilia na kutathmini athri za uchafuzi wa mazingira katika makazi, viwanda, migodi, ujenzi, biashara, kilimo na ufugaji.
3. Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Environmental Impact Assessment)
i.Kuandaa tathmini ya kimkakati kwa mazingira kwa mipango na program za Halmashauri zinazotakiwa kufanyiwa tathmini hiyo kama zilivyobainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni zake;
ii.Kufuatilia utekelezaji wa utaratibu wa Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira katika maeneo yao na kutoa ushauri kwa Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais;
iii.Kufuatilia utekelezaji wa utaratibu wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) katika maeneo yao kwa shughuli zinazotakiwa kufaniwa TAM kama zilivyobainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni zake;
iv.Kufuatilia utekelezaji wa Mpango na Masharti ya TAM kwa kila shughuli / mradi uliofanyiwa tathmini hiyo au kukaguliwa na kutoa ushauri kwa Mkurugenzi MKuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira;
v.Kushirikisha umma katika maamuzi yanayoweza kuathiri mazingira na katika uandaaji wa Sera, Mikakati, Mipango, Programu na Sheria zinazohusu mazingira katika maeneo yao;
vi.Kufanya utafiti/uchunguzi wa uharibifu au athari kwa mazingira unaosabishwa na shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimammizi wa Mazingira;
vii.Kufuatilia na kutoa ushauri kuhusu maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizoendelevu kama vile uchimbaji madini holela, uvuvi haramu, kilimo kisicho kuwa endelevu, ujenzi haolela, ufugaji wa kuhamahama usiozingatia uwezo wa malisho n.k;
viii.Kusimamia / kuratibu utekelezaji wa kazi za Kamati za Mazingira na Kamati za Halmashauri zinazoanzishwa na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ngazi ya Halmashauri hadi Kitongoji / Mtaa;
ix.Kuandaa na kutekeleza mikakati wa Kitaifa wa Kuhimili na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi;
x.Kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango na programu za Halmashauri kwa kuzingatia Programu ya Kitaifa ya Kukabiliana na Kuenea kwa ahli ya Jangwa na Ukame;
xi.Kuandaa nyezo kutoa elimu ya mazingira kwa jamii kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni zake, mikakati ya kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, mikakati ya kukabiliana na kuenea kwa hali ya jangwa na Ukame;
xii.Kuandaa nyezo na kutoa elimu ya mazingira kwa jamii kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni zake, mikakati ya kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, mikakati ya kukabiliana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame;
xiii.Kutekeleza mikakati, mipango na program ya Mikataba ya Kimataifa na Kanda ya mazingira inayohusiana na kemikali, taka za sumu na udhibiti wa uchafuzi;
xiv.Kusimamia utekelezaji wa Maagizo ya kimkakati yanayotolewa na Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira na kutoa taarifa za utekelezaji kwa Mamlaka husika.
xv.Kusimamia na kutekeleza Sera ya Taifa ya Mazingira, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kuhusu masuala ya udhibiti wa Kanuni, Miongozo, Mikakati, Mipango na Program za Kisekta; na
xvi.Kusimamia na kutekeleza kazi nyingine zitakazoelekezwa na Mamlaka ya juu.
IIUDHIBITI TAKA NGUMU:
i.Usafishaji na Ukusanyaji wa Taka Ngumu kutoka kwenye majengo, maeneo ya
wazi, barabara na Mifereji ya kuondoa maji ya Mvua (Cleaning of Buildings, Open Spaces, Roads and Drainages)
\Kuweka mifumo na miundombinu isiyoathiri afya na mazingir ya usimamizi wa taka kuanzia zinapozalishwa hadi zinapotupwa kwa kuzingatia utenganishaj, ukusanyaji na uhifadhi, urejelezaji, utekelezaji katika matanuru maaalumu na utupaji katika madampo ya kisasa;
ii.Kubuni mbinu za kupunguza taka na kusmamia utekelezaji wake ili kupunguza uchafuzi wa mazingira;
iii.Kufanya tafiti / uchunguzi ili kubaini aina ya taka zinazozalishwa kutoka katika masoko, makazi, maeneo ya biashara na taasisi na kubuni njia bora za kupunguza, kutenganisha, kuhifadhi na kutupa taka;
iv.Kusimamia usafi katika mifereji ya kukusanya maji ya mvua na kuhakikisha inafanya kazi muda wote;
2. Uhifadhi wa muda, Uchambuzi na Usafirishaji Taka Ngumu (Solid Waste Storage; Sorting, Transportation)
i.Kuweka na kusimamia miongozi ya usimamizi wa taka ngumu katika miundombinu ya kuhifadhi, kusafirisha na kuteketeza na kutupa taka ngumu kwa kushirikiana na Mamlaka husika.
ii.Kuandaa na kusimamia miongozi ya kutenga maeneo kwa ajili ya kukusanya taka kwa muda ili kuhakikisha kuwa yana ukubwa wa kutosha na kudhibiti athari kwa jamii, afya na mazingira;
iii.Kutenga maeneo maalum ya kuanzisha vituo vya kukusanya, kuchakata na kuhifadhi taka zitakazo na vifaa vya umeme na elektroniki, mafuta machafu na taka nyingine za sumu;
iv.Kutoa amri inayowataka wenye viwanda na maeneo ya biashara kutenga maeneo ya kutosha, kuweka vifaa vya kutenganisha na kuhifadhi taka, mitambo ya kurejeleza na kurudufu taka ngumu; na
v.Kuweka vyombo vya kuhifadhi taka katika maeneo yote ya umma na kuhakiki usafi wa maeneo hayo;
3. Uchambuaji, Utupaji taka Ngumu na Uendeshaji Dampo la Kisasa (Sorting and Sanitary Disposal of Solid Waste and Dumpsite Management)
i.Kuanisha na kutenga maeneo maalum na a kutosha kwa ajili ya ujenzi wa dampo za kisasa;
ii.Kuweka na kusimamia miongozi ya utupaji wa mwisho wa taka ngumu na uendeshaji wa dampo za kisasa;
iii.Kuweka tozo ya usimamizi wa taka inayozingatia gharama halisi ya huduma katika ukusanyaji hadi utupaji katika madampo ya kisasa; na
iv.Kutoa amri za kuzuia utupaji ovyo wa taka wa aina zote katika fukwe, maeneo ya wazi, mito na mifereji ya maji ya mvua;
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi