Mshauri Mkuu wa masuala yote ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu katika Halmashauri.
Kuratibu na kusimamia Ajira zote katika Manispaa (mpya, mbadala na mikataba).
Kusimamia upandishwaji vyeo na uthibitishaji kazini watumishi.
Kusimamia masuala ya fedha katika Idara.
Kusimamia nidhamu kwa watumishi na kuwa katibu wa Kamati ya Uadilifu ya Halmashauri na Kamati ya Maadili ya Madiwani.
Kusimamia uandaaji wa bajeti ya mishahara na Ikama ya watumishi wote wa Manispaa na bajeti ya Idara kwa ujumla.
Kusimamia na kushughulika mafao ya wastaafu.
Kusimamia utekelezaji wa upimaji utendaji kazi kwa njia ya (OPRAS).
Kushughulikia majibu ya barua zote toka TAMISEMI, OR-MUU, TUU, RAS na mamlaka zingine za juu.
Kuhakiki orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi katika Idara.
Kushughulikia majibu ya yatokanayo na kikao cha baraza la Halmashauri, Kamati za kudumu za Halmashauri na CMT.
Kuratibu na kusimamia kazi nyingine zote zitakazofanywa na maafisa utumishi wengine, waandishi wa vikao vya halmashauri na afisa usafirishaji pamoja na mwangalizi wa ofisi.
Kuwa mlezi wa kata kadri itakavyopangwa na Mkurugenzi wa Manispaa.
Kushughulikia maslahi ya watumishi wote wa Halmashauri na Wah.madiwani.