WAJIBU WA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII KWA WANANCHI
Idara ya Maendeleo ya Jamii inawajibik kwa wananchi wa Manispaa ya Moshi kama ifuatavyo:
1.Kusaidia jamii kupata ujuzi wa aina mbalimbali ambao katika eneo wanaloishi. Ujuzi huo utawasaidia kuuinua kiwango cha kipato chao na kuleta mabadiliko yanayoweza kupimika katika Maisha yao ya kila siku.
2.Kuhamasisha/kushawishi ushirikiano wa kudumu na wa karibu wa mamlaka zote zinazohusika kuchangia kwa hali na mali maendeleo ya jamii.
3.Kusaidia kupanga na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya jamii.
4.Kuimarisha jamii ili itambue kuwa rasilimali za kuleta maendeleo zipo ndani yao wenyewe na kwamba wana uwezo wa kuzibaini na kuzitumia na mafanikio yakaonekana bila kutegemea msaada kutoka nje.
5.Kusaidia kuhakikisha kuwa sera za uchumi/ mapato zilizop au ziliwekwa mamlaka husika zinatumika katika kuleta maendeleo ya jamii.
6.Kusaidia kujenga ari miongoni mwa jamii na kusisitiza itambue kuwa familia/ kaya ndiyo msingi mkuu wa maendeleo ya jamii na ndipo hapo mzanzo wa Maisha bora utakapoanza kuonekana kwa kufanya kazi kwa bidi.
7.Kusaidia katika kuhakikisha kuwa mipango ya utekelezaji inayosimamiwa na sekta ya maendeleo ya jamii imebuniwa na jamii yenyewe na tathmini inafanywa na wao wenyewe pia
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi