Kitengo cha ukaguzi wa ndani ambacho kimeanzishwa chini yakifungu 45(1) cha sheria ya fedha ya mamlakayaserikalizaMitaana 13 yamwaka 1982(section 45(1) of local authority finances act) ni moja kati ya vitengo vilivyopo katika Halmashauri. Kitengo cha ukaguzi kinakuwa na majukumu ya kukagua, kusimamia na kushauri mambo ya fedha na mfumo wa Halmashauri kwa ujumla kuhakikisha maslahi ya Halmashauri yanalindwa na kumshauri Afisa masuuli juu ya matumizi bora ya fedha za serikali na mfumo mzima wa Halmashauri kwa ujumla. Kitengo cha ukaguziwa ndani katika Halmasahuri ya Moshi Manispaa kina watumishi Watano
KAZI NA MAJUKUMU YA KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI
Kufanya ufuatiliaji na Ukaguzi na usimamizi wa fedha zote zinazokusanywa zinazopokelewa na Halmashauri
Kuhakikisha kuwa sera za matumizi ya fedha za serikali zinafuatwa kikamilifu kama zilivyohainishwa kwenye mamlaka za serikali za mitaa na sera nyinginezo za matumizi ya fedha.
Kufanya Ukaguzi wa matumizi ya ankra zote za Halmashauri kila robo mwaka na kuandaa ripoti kwa afisa masuuli kabla ya tarehe 15 ya mwezi unaofuata robo husika.
Kufanya ukaguzi wa miradi na mali zote za Halmashauri na kuhakiki uwepo thamani ya fedha (Value for money )
Kupitia na kuangalia utendaji na mfumo wa kilasi kuwa halmashauri na kuangalia kama utekelezaji.
Kuandaa mpango kazi wa kitengo cha ukaguzi na kuuwasilisha katika kamati ya ukaguzi na kwa Afisa Masuuli.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi