• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Moshi Municipal Council
Moshi Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • History
      • Maadili ya Msingi
    • Dira na Dhamira
      • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
        • Elimu ya awali na Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji na Ardhi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Mipango Takwiku na Ufuatiliaji
      • Afya Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Elimu ya awali na Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ununuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Election
    • Muundo wa Kiutawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Michezo na Utamaduni
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipango Miji
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kamati ya Fedha na Uongozi

 
 KAMATI YA FEDHA, UTAWALA
Majukumu ya Jumla:                  
Kamati hii inawashirikisha wenyeviti wa kamati zote za kudumu na inapaswa kukutana kila mwezi mara moja.  Aidha, madaraka ya kamati hii ni kama ya kamati zingine za kudumu na hivyo hairuhusiwi kisheria kufanya kazi/majukumu ya kamati nyingine za kudumu.  Kwa ujumla, majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali ya Halmashauri kwa kupitia vikao vyake.
Majukumu maalum ya Kamati:
  • Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato;
  • Kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango wa maendeleo kwenye Halmashauri ili kuidhinishwa na halmashauri;
  • Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri, ukusanyaji wa mapato, kufuta madeni, na kuomba vibali maalum kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye Dhamana ya Serikali za Mitaa;
  • Kufikiria na pale inapowezekana, kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu sheria ndogo na utendaji katika ngazi za chini za Halmashauri;
  • Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya Fedha (Re-allocation) yaliyopo katika makisio yaliyoidhinishwa na kuyapeleka kwa Halmashauri;
  • Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye Kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawaislisha kwenye Halmashauri;
  • Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauri mikopo yote ya Halmashauri;
  • Kupokea na kujadili taarifa za wakaguzi wa fedha na mali ya Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa sheria za Serikali za Mitaa Sura ya 290;
  • Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za halmashauri, kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Waziri na taratibu nyingine zitakazowekwa na Halmashauri;
  • Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususani kuhusu taratibu za fedha, ikiwa ni pamoja ya mapitio ya mara kwa mara yanayohusu thamani ya fedha ambapo kanuni mbalimbali za manunuzi ya mali na vifaa hutumika;
  • Kufikiria na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali, vinavyotolewa na halmashauri;
  • Kufikiria mapendekezo ya bajeti na mipango ya maendeleo ya kila kamati ya kudumu na kuiwakilisha kwenye halmashauri ili kupata idhini;
  • Kushughulikia tofauti ya mapato na matumizi katika bajeti yote na kupendekeza hatua stahiki ya kuchukua na kuondoa mapungufu katika mapato au ziada matumizi;
  • Kufikiria mapendekezo yote yanayohusu matumizi makubwa ya fedha kabla hayajawasilishwa kwenye halmashauri ili kupata idhini;
  • Kupokea mahesabu ya nwaka ya halmashauri na kuhakikisha taarifa za mahesabu ya mwaka inawasilishwa kwa wakati kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali;
  • Kupitia na kuidhinisha mpango wa manunuzi ya halmashauri  kwa kuzingatia mpango wa bajeti uliopitishwa na halmashauri;
  • Kupitia taarifa ya kila robo mwaka kuhusu manunuzi iliyowasilishwa na Afisa masuuli;
  • kusimamia utekelezaji wa mikataba ya halmashauri kwa kukagua miradi inayotekelezwa na vifaa vilivyopokelewa;
  • Kumwelekeza mkurugenzi kufanya manunuzi au ukaguzi wa huduma au vifaa vilivyonununliwa ili kupata thamani halisi, itafanyika hivyo endapo itadhirika kwamba, maelezo yaliyotolewa kuhusu manunuzi ya vifaa au huduma hayaridhishi;
  • Kuidhinisha majina ya wajumbe wa Bodi ya zabuni na wa Bodi zingine kwa mujibu wa sheria husika;
  • Kushughulikia orodha ya wadaiwa wote itakayowasilishwa kwenye kamati na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;
  • Kupendekeza njia na taratibu za kuondosha vifaa chakavu. Uondoshaji wa vifaa unaweza kufanyika kwa njia ya kuuza au kuviharibu.
  • Kujadili na kupitia taarifa za fedha za kila mwezi na kila robo mwaka;
  • Kupendekeza kwa halmashauri hatua za kuchukua kuhusu kufuta madeni ya Halmashauri;
  • Kushughulikia sera kuhusu kukopa na uwekezaji;
  • Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na halmashauri nyingine;
  • Kurekebisha na kusimamia makusanyo na matumizi ya mapato ya vijiji na miji midogo kwa mujibu wa sheria;
  • Kuteua wakaguzi wa fedha/mali za serikali kwa mujibu wa sheria, sura (290).
  • Kujadili na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kuhusu mambo yote ya nayohusu masuala ya ajira na kinidhamu ya wafanyakazi na watumishi.
  • Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu nyumba za Halmashauri.
  • Kupokea na kutoa uamuzi juu ya mapendekezo ya watumishi wanaokenda masomoni.
  • Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi, ikiwa ni pamoja na mikopo, nyumba, usafiri, matibabu, rambirambi na motisha nyinginezo.
  • Kupitisha mapendekezo ya kuthibitisha watumishi kazini baada ya kumaliza kipindi cha majaribio kulingana na miundo husika ya utumishi.
 

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA MANISPAA YA MOSHI April 17, 2025
  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA YA MOSHI July 13, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MUDA YA KUSIMAMIA UCHAGUZI MKUU September 21, 2020
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA(JOINING INSTRUCTIONS)KIDATO CHA KWANZA SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA YA MOSHI 2021 December 18, 2020
  • Tazama

Habari Mpya

  • ZAWADI YA USAFI YARUDI NYUMBANI

    April 10, 2025
  • BAJETI YA KIMKAKATI WA KUONGEZA MAPATO YA NDANI

    February 07, 2025
  • MAMA SAMIA ATOA TSH. BILLIONI 956 KWA AJILI MIRADI YA MAENDELEOA MKOA WA KILIMANJARO

    January 27, 2025
  • MANISPAA YATOA MIKIPO ISIYO NA RIBA ZAIDI YA TSH. BILLION 1.1

    January 20, 2025
  • Tazama

video

ZAWADI YA USAFI YARUDI NYUMBANI
videos

Kurasa za Karibu

  • Instagram account

Tovuti Mashuhuri

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    MOSHI MANISPAA KILIMANJARO

    Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI

    Simu: +255-027-2752906

    simu ya Mkononi: +255-027-274371/4

    Barua Pepe: md@moshimc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi