Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Moshi Mjini, Wakili Sifael Kulanga, amewataka wasimamizi wasaidizi wa ngazi ya kata kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa bidii, uadilifu na kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa kata, Wakili Kulanga alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa weledi na uwazi.
Alisisitiza kuwa utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia taratibu utasaidia kuimarisha imani ya wananchi katika mchakato wa uchaguzi na kuhakikisha haki inatendeka kwa pande zote
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi