1.0 UTANGULIZI
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ulianza Mwezi Julai, 2015 ambapo jumla ya Kaya 2691 zilitambuliwa na kuthibitishwa na mikutano ya wananchi wa mitaa husika. Halmashauri ya Manispaa ya Moshi inatekeleza kipengele kimoja cha mpango ambacho ni Uhawilishaji wa Fedha. Kaya 2691 zilianza uhawilishaji wa fedha kipindi cha Julai, 2015 hadi sasa jumla ya kaya 1490 zimesalia baada ya kaya zingine kuondolewa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo na kuhama kwa walengwa.
2.0 UHAWILISHAJI WA FEDHA KWA KAYA MASKINI.
Manispaa ya Moshi kupitia TASAF awamu ya tatu imepokea jumla ya kiasi cha fedha 1,370,868,022.94 katika kipengele cha uhawilishaji fedha kimefanyika kwa mizunguko 15 na jumla ya TZS 1,223,577,977.27 zimeawilishwa kwa walengwa waliopo katika mpango kwa mitaa 35. Kiasi kilichobaki ni kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za Mpango.
3.0 MAFANIKIO
Kuboreka kwa lishe kutoka lishe duni kwenda lishe bora na idadi ya milo toka mmoja hadi mitatu na zaidi kwa Kaya.
Kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni na Mahudhurio ya watoto Kliniki kutokana na ruzuku ya utimizaji wa masharti ya elimu na afya
Kaya Maskini kuchangia na kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (TIKA), CHF jumla ya kaya 649.
Walengwa 673 wanajishughulisha na biashara ndogondogo, walengwa 309 wanajishughulisha na kilimo, 256 wanajishughulisha na ufugaji na walengwa 163 wamejiunga na vikundi vya kuweka na kukopa.
Walengwa kupata elimu kupitia maafisa ugani inayohusiana na Kilimo,ufugaji na Lishe katika kila dirisha la Malipo.
4.0 CHANGAMOTO
Baadhi ya wazazi kutaja majina ya watoto ambayo hayatumiki shuleni hivyo kusababisha usumbufu kwa ujazaji wa fomu za utimizaji wa masharti ya elimu na afya.
Kukosekana kwa mtandao baadhi ya muda kunapelekea kuchelewa kwa malipo ya walengwa.
Malalamiko ya wananchi wanaotaka kuwemo katika mpango ili waweze kunufaika na mpango.
5.0 MIKAKATI YA KUTATUA CHANGAMOTO
Wazazi wameelimishwa kutoa taarifa sahihi ili kusaidia kurekebisha taarifa za watoto na kufanikisha lengo la utimizaji wa masharti ya afya na elimu.
Mawasiliano na Mtaalam wa mifumo ngazi ya Halmashauri,Mkoa na TAMISEMI ili kutatua tatizo la mtandao.
Mawasiliano na TASAF Makao Makuu ili waweze kufanya zoezi la utambuzi upya kwa kaya ambazo hazipo katika mpango.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi