Idara ya Afya ina jukumu la kuhakikisha kuwa watoa huduma za Afya Manispaa wanatoa huduma bora zenye lengo la kuboresha, kulinda, kuendeleza na kudumisha Afya za wakazi wa Halmashauri hii. Idara inatekeleza majukumu yake kupitia vitengo vyake viwili vya Kinga na Tiba.
KINGA:
Kitengo hiki kinahusika na uzuiaji wa kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza katika jamii. Magonjwa ya kuambukiza ni yale yanayoweza kuenea toka kwa mtu mmoja hadi mwingine kama kuhara, kuhara damu, kipindupindu, homa ya matumbo n.k. Pia, kinahusika katika kuthibiti kuwepo kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, magonjwa ya moyo katika jamii. Kitengo pia hufanya usimamizi wa sheria za usafi wa mazingira, vyakula na za mji (Public Health Act) pamoja na uzuiaji kuenea kwa magonjwa ya milipuko/kuambukiza.
TIBA:
Kutoa matibabu, vipimo na madawa. Huduma hizo hutolewa kwa jamii kwa ushirikiano (public private partnership) kupitia vituo 54 vya serikali, taasisi, binafsi kwa faida na bila faida vilivyoko katika kata 21 za Manispaa.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi