Kazi za Mipangomiji na usimamizi wa Ardhi katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi zinasimamiwa na kutekelezwa na Idara ya Mipangomiji na Ardhi. Ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yake Idara imegawanyika katika vitengo vinne ambavyo ni Mipangomiji, Ardhi, Uthamini na Upimaji.
Kitengo cha Mipangomiji kinajihusisha na kazi za maandalizi ya mipango ya kina ambayo huwezesha kupatikana kwa maeneo kwa ajili ya makazi, biashara, maeneo ya wazi, huduma za jamii, maendeleo ya viwanda, miundombinu na maeneo ya hifadhi. Pia kitengo kinafanya kazi ya usimamizi wa matumizi ya ardhi kwa mujibu wa mipango, kuanisha maeneo mapya ya mipango na utunzaji wa maeneo ya wazi.
Kitengo cha Ardhi kinajihushisha na utawala na usimamizi wa ardhi yote iliyopo ndani ya eneo la utawala wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa kuzingatia sheria za ardhi na sheria ndogo za Halmashauri .
Kitengo cha Uthamini kinafanya kazi ya kukusanya, kufanya uthamini na kuhifadhi taarifa muhimu zinazohusu soko la ardhi ndani ya Manispaa, pia kitengo hiki kinafanya kazi ya uthamini wa ardhi kwa lengo la kutoa fidia, kuuza, dhamana na kwa malengo ya utozaji kodi.
Kitengo cha Upimaji kinafanya kazi za upimaji na uchoraji ramani za viwanja kwa ajili ya maandalizi ya hati za viwanja.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi