TIBA:
•Tunafanya uchunguzi/vipimo mbalimbali vya magonjwa.
•Tunagundua magonjwa yanayoathiri jamii.
•Tunatoa matibabu magonjwa utoaji dawa, uzalishaji, upasuaji na mazoezi.
•Tunahakikisha madawa, vifaa tiba, vitendanishi vinapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya.
•Tunasimamia ubora wa huduma zitolewazo Manispaa.
•Tunatathmini matokeo ya huduma mbalimbali.
•Tunatafiti magonjwa mbalimbali yaliyo katika eneo letu.
•Tunasimamia sera viwango na miongozo mbalimbali ya matibabu.
•Tunatoa mafunzo kwa watoa huduma za tiba na kuwapatia vitendea kazi.
•Tunatoa matibabu kwa magonjwa ya akili, uzazi, upasuaji, watoto, na magonjwa ya watu wazima ya kawaida, Tiba ya meno, macho nk.
•Tunasimamia matibabu katika kliniki mbalimbali kama ukimwi, kifua kikuu.
•Tunatoa huduma za kiuuguzi (Nursing care) kwa wagonjwa waliolazwa nk.
•Tunasimamia tiba asili na mbadala.
Kinga:
•Tunatoa elimu ya Afya kuhusu kinga kwa ajili ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na yasiyoambukiza.
•Tunatoa chanjo mbalimbali hasa kwa watoto chini ya miaka 5.
•Tunadhibiti magonjwa mbalimbali ya mlipuko kama Kipindupindu, Ebola, Dengue fever na magonjwa mengine ya kuharisha malaria nk.
•Tunasimamia usafi wa mazingira hasa vyoo na matumizi yake, usafi na usalama wa maji na usafi binafsi.
•Tunafanya ukaguzi, na usimamizi wa shughuli za kinga wa vyakula mbalimbali.
•Tunashirikiana na kitengo cha Afya ya uzazi na mtoto (RCH) katika utoaji wa huduma.
•Tunatoa elimu za afya mashuleni,kazini na kwenye jamii
•Tunakagua ramani za majengo na majengo
•Tunatoa dawa kwa magonjwa yasiopewa kipaumbele(NTDs)
•Tunasimamia sheria za Afya.
oThe Tanzania Food, Drugs and Cosmetics Act 2003.
oThe Public Health Act 2006
oLocal govt (Urban Authorities Act 1982)
oInternational Notifiable Diseases (Prevention) Act 1964 (Act No. 3 of 1964)
oEnvironmental management Act, 2004
oSheria ndogo ya Manispa ya Moshi ya mwaka 2006
•Tunakagua na kuchukua sampuli za maji safi ili kulinda ubora na usalama wake.
•Tunakagua maeneo ya kazi ili kuona kwamba afya mahali pa kazi inazingatiwa.
•Tukagua na kushauri juu ya udhibiti wa taka ngumu pamoja na taka miminika.
•Tunakusanya takwimu za magonjwa ya kuambukiza.
•Tunaendesha mashtaka mahakamani kwa wavunja sheria za Afya.
Lishe:
•Tunatoa elimu na kuhamasisha kuhusu lishe bora na ulaji unaofaa kwa jamii.
•Tunaendesha kampeni ya vitamin A na kutoa dawa za minyoo kwa watoto chini ya miaka 5 ambayo hufanyika mara 2 kwa mwaka (Juni na Desemba).
•Tunaendesha upimaji wa Afya za jamii kwa kuchukua uzito na urefu, uzito kwa umri na kupima mzunguko wa mkono.
•Tunatoa huduma za masuala ya lishe katika kliniki za CTC na kisukari
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi