Baraza la Madiwani la Manispaa ya Moshi kwa kauli moja limepitisha mpango na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 kwa jumla ya Tshs 50,639,993,000
Mstahiki Meya wa Manispaa Mhandisi Zuberi Kidumo, alitangaza bajeti hiyo , wakati akifunga kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili na kuidhinisha mapendekezo ya bajeti na kueleaza kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Shs 8,091,260,000, Matumizi ya kawaida (OC) ni Shs 743,409,000, Miradi ya Maendeleo ni Shs 9,792,485,000 na kwa upande wa Mishahara inatarajiwa kuwa Shs 32,012,839,000 hivyo kufanya jumla ya Bajeti ya Manispaa ya Moshi kuwa Shs .50,639,993,000.
“Manispaa ya Moshi inahikikisha kuwa inatekeleza ila ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 na imejipanga kuweka nguvu zake zaidi katika ukusanyaji mapato na kusimamia miradi miradi ya maendeleo ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi na wakazi wa Manispaa ya Moshi”alisema Mhandisi Zuberi
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi