Halmashauri ya manispaa ya Moshi,imetoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya shilingi milioni 225 kwa vikundi 45 vikiwemo vikundi 38 vya wanawake, 5 vya vijana na vikundi 2 walemavu, katika manispaa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2018/2019.
Hayo yameelezwa na mkuu wa Idara Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii Rose Minja, wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Ths million 97 kwa ajili ya mikopo hiyo kwa vikundi 16 vya wanawake vikundi 3 vya vijana kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halamshauri, Minja alisema zoezi utoaji wa mikopo hii isiyo na riba limezingatia masharti ya utoaji wa mikipo ambapo vikundi vyote ni lazima viombe mikopo kupitia kata husika na kuhakikisha vinatambuliwa na kata hiyo.Vile vile Idara inaangalia historia ya kikundi husika kujiridhisha uendeshaji wa kukundi hichi(VICOBA) kama kina uwezi wa kukopa na kurejesha. Licha ya kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa vikundi kujitokeza na kuomba mikopo lakini vijana wameonekana kukosa muamko wa kujiunga katika vikundi na kupelekea kukosa fursa ya kupatiwa mikopo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, alitoa wito kwa wanufaika wa mikopo hiyo kuhakikisha kuwa fedha wanayopewa inakwenda kutekeleza miradi /biashara walizokusidia na kujenga tabia ya kuzirejesha kwa wakati ili ziweze kunufaisha vikundi vingi zaidi kama inavyotarajiwa.
“Nyinyi leo mnanufaika na mikopo hii isiyo na riba inayotolewa na serikali na mnayo nafasi kubwa ya kujikwamua kiuchumi na kuzisaidia familia zenu pamoja na kuhakikisha kuwa Manispaa na Wilaya yetu ya Moshi inakuwa kiuchumi.Tunategemea baada ya muda mfupi mtakuwa kiuchumi na sisi tutahikisha tunawaunganisha na taasisi kubwa za kifedha ili muweze kukopa fedha zaidi .”,alisema na kuongeza tunaona kina mama mmekuwa mstari wa mbele katika kujitokeza kuomba mikopo naomba muwasaidia na vijana wenu ili waweze kujikwamua kiuchumi nao wahimizeni wajiunge kwenye vikundi kwa ajili ya kuwa na sifa ya kukopesheka.
Awali, Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Danfrod Kamenya, alisema Manispaa imeendelea kuhamasisha wanawake,Vijana na Walemavu kujiunga katika vikundi ili kupata fursa ya kupata mikopo isiyo na riba kutokana na asilimia kumi inayotengwa na Halmashauri kila mwaka kutokona na mapato ya ndani lakini tatizo limekuwa kubwa hasa kwa vijana wa kiume kutokuwa na muamko wa kufanya kazi katika vikudi. Hata hivyo Manispaa kwa kushirikiana na wadau inaendelea kuhamasisha vijana wa kiume wajiunge kweny vikundi na kufanya kazi kwa kushirikiana.
Hatibu Hamad kutoka kwenye moja ya vikundi vya vijana vilivyonufaika na mkopo anasema vijana wengi wamekuwa wakikosa sifa ya kupatiwa mikopo kutokana na kutopenda kujiunga katika vikundi, huku wengi wakiwa hawana makazi maalumu.
Nao wanufaika wa mikopo hiyo wameishuruku Serikali ya awamu ya tano inayongozwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John P. Magufuli kwa kuwajali na kuwawezesha wananchi hali ya chini hasa wajasiriamali wadogo kutoka kwenye vikundi(VICOBA) kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba na wameahidi kuitumia mikopo hiyo vizuri ili kutimiza lengo la serikali la kuwakwamua kiuchumi.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi