Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,imetoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya shilingi milioni 100 kwa vikundi 18 vikiwemo vikundi 9 vya wanawake,7 vya vijana na vikundi 2 wenye ulemavu, Manispaa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2019/2020.
Hayo yameelezwa na mkuu wa Idara Maendeleo ya Jamii Rose Minja, wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Ths million 100 kwa ajili ya mikopo hiyo kwa vikundi 18 vya wanawake,Vijana na wenye ulemavu.
Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmshauri, Minja alisema zoezi utoaji wa mikopo hii isiyo na riba limezingatia sheria ya Fedha ya serikali za Mitaa sura 290. Na kanuni za utoaji na usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake ,Vijana na Watu wenye Ulemavu kifungu 37A (4) za mwaka 2019 na kanuni zake iliyotangazwa katika gazeti la Serikali Na.286 la tarehe 5/4/2019.
“Sifa za kupata mkopo ni kuwa vikundi vya Wanawake idadi ya wanakikundi wawe 10 na kuendelea,Vijana kinatakiwa kiwe na Vijana 10 na watu wenye Ulemavu wanatakiwa wasio chini ya watu 5.Vikundi hivi havitajumuisha wajumbe wenye ajira rasmi na wanatakiwa wawe na mradi wa pamoja”.Alisema Rose
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, alitoa wito kwa wanufaika wa mikopo hiyo kuwa kuhakikisha kuwa kama wanaona mambo sio mazuri katika uendeshaji wa mradi waliochagua wanatakiwa wasisite kuomba ushauri kwa wataalamu wa Manispaa kama vile Afisa biashara na Mchumi ili kuhakikisha wanafanikiwa malengo waliojiwekea.
“Sina wasiwasi na wakinamama kwani huwa wanaambizana wakati wanaona mambo hayaendi vizuri au mmoja wao anawakwamisha lakini kwa Vijana jambo hilo mara nyingi huwa halifanyiki.Nawasihi Vijana kuhakikisha kuwa mnakwenda pamoja katika uendeshaji wa miradi na mtumie muda wenu mwingi kushirikiana na kukumbushana ili mfanikiwe kwa pamoja”.,alisema na kuongeza Vijana tushikamane pamoja ili tufanikiwe na kufanikisha mlichokusudia ili kuonyesha shukrani kwa Serikali ya CCM na awamu Tano kuwa imewajali na imewakwamua kwa kuwapa mikopo hii isiyokuwa na riba.
Awali, Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Lainie Kamendu, alisema Manispaa imeendelea kuhamasisha wanawake,Vijana na Walemavu kujiunga katika vikundi ili kupata fursa ya kupata mikopo isiyo na riba kutokana na asilimia kumi inayotengwa na Halmashauri kila mwaka kutokona na mapato ya ndani robo ya pili Halmashauri inayo kiasi cha Tsh. Milion 300 ila kwa siku hii ya leo tunatoa mikopo yenye thamani ya Tsh million 100 na baada ya wiki mbili mchakato mwingine utakuwa umekamilika na tunatarajia kutoa mikopo mingine yenye thamni ya Tsh. Million 200.
Nao wanufaika wa mikopo hiyo wameishuruku Serikali ya awamu ya tano inayongozwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John P. Magufuli kwa kuwajali na kutunga sheria iliyoboresha utoaji wa mikopo kwa Wajasiriamali wadogo wenye mradi mmoja .Kwasasa sisi tunamradi mmoja tunaoundesha kwa pamoaj hivyo ni rahisi sisi kurejesha mkopo kwani tunafanya kazi pamoja na sio kama mwanzo tulikuwa chukua fedha kama kikundi na kila mmoja anafanya shughuli yake na kuleta shida wakati wa marejesho.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi