Wajumbe wa Kamati ya Fedha wa Kamati ya Fedha na Uongozi Halmshauri ya Manispaa ya Moshi leo tarehe 18/07/2023 wamekagua miradi 4 ya ujenzi yenye thamani ya Tsh. 1.657 fedha kutoka Serikali Kuu.
Miradi hiyo ni Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi katika Kata ya Pasua, Ujenzi wa Miundombinu Shule ya Sekondari Moshi, Ukarabati wa Miundombinu ya Shule kongwe ya Msingi Muungano na Ujenzi wa Ukuta na Ukarabati wa Jengo la Halmashauri ya Ofisi za Halmashauri. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi ameridhishwa na utekezwaaji wa mradi hiyo na amewapongeza watalam wa Halmashauri kwa usimamizi wa mradi hiyo na kuwataka kufanyia kazi ushauri uliotolewa na madiwani.
Naye Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Mhe Priscus Tarimo kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Moshi Mjini ameishukuru Serikali Awamu ya Sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhi Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuleta Fedha za miradi ya Maendeleo.
"Tunaishukuru sana Serikali kwa kutuletea fedha za miradi na tunahakika miradi hii itapokamilika itaboresha mazingira ya ufundishaji pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi wa Halmashuri ya Manispaa ya Moshi" Alisema Mhe Tarimo
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi