Halmashauri ya Manispaa ya Moshi , imetoa mkopo
wa Shilingi Milioni189, kwa vikundi 38 vya wanawake na vijana,lengo
likiwa nikuwawezesha kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo na
kujikwamua kiuchumi.
Mbali na mikop hiyo, pia imetoa vitambulisho maalumu vya matibabu bure
kwa wazee 1,000, hatua ambayo itawawezesha kupata matibabu bure katika
vituo vya afya na Hospitali ya Wilaya.
Akizungumza jana wakati wa utoaji hundi kwa vikundi hivyo na kadi za
matibabu kwa wazee, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Michael Mwandezi,
alisema katika mwaka wa fedha 2017/18, Halmashauri hiyo imetenga
zaidi ya Shilingi 557.2 Milion,kutoka katika mapato yake ya ndani kwa
ajili ya vikundi vya kinamama na vijana.
Alisema mpaka sasa wameshatoa mikopo kwa vikundi 44, na saccos Moja,
ambapo awamu ya kwanza walitoa 45Mlion,kwa vikundi Viwili vya vijana
na vikundi Saba vya wanawake na kwamba Mikipo iliyotolewa ya Shilingi
189Milion,ni awamu ya Pili.
“Tunatarajia vijana na kina mama baada ya kupata fedha hizi, wanaingia
mtaani kufanya shughuli mbalimbali ambazo zitawaongezea kipato na
kujikwamua kiuchumi”
Akizungumzia Vitambulisho vya matibabu kwa wazee, Mwandezi alisema
kulingana na Takwimu zilizokusanywa katika Kata 21,Manispaa hiyo ina
jumla ya zawee 4,319 na kati ya hao 2112 ni wahitaji.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, mbali na
kuupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kutekeleza vyema mipango ya
serikali,alivitaka vikundi vyote vilivyopata mikopo, kuitumia kwa
malengo yaliyokusudiwa, ili kufanikiwa kuirejesha kwa wakati na kutoa
fursa kwa wengine kunufaika na fedha hizo.
Awali akizungumza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya,
alisema, Manispaa hiyo imekuwa ikijitahidi kutenga na kutoa fedha
kutoka katika mapato yake ya ndani kwa ajili ya vijana na kina mama,
kama wanavyoelekezwa na serikali.
Mboya aliwataka viongozi wa vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo,
kusimamia kwa uaminifu, ili kuwezesha kurejeshwa kwa wakati, na
kuwasaidia wengi zaidi na kufanikisha jitihada za kujikwamua kiuchumi.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi