Matokeo chanya katika uwajibikaji,usimimamizi mzuri na uwazi kwa serikali ya awamu ya tano, umeiwezesha Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kutekeleza mradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za lami na madaraja, iliyogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 29.82 zilizotolewa na Serikali kuu.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabaraba,madaraja na vivuko Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Moshi Michael Mwandezi, Alisema kuwa katika kipindi kisichozidi miaka mitatu kuanzia mwaka 2015 hadi 2018, Manispaa hiyo imetengeneza jumla ya kilomita 29.3 za barabara za kiwango cha lami, madaraja mawili na vivuko vinne.
“Katika utawala wa serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais Dk.John Magufuli tumejenga barabara zenye urefu wa kilomita 13.2 kwa fedha zilizotokana na Mfuko wa Barabara na kilomita 16.575 kwa fedha za Mradi wa ULGSP, ambao ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia,”alisema Mwandezi.
ULSGP ni Mradi wa Uimarishaji Halmashauri za Miji katika Utoaji wa Huduma unaosimamiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaopo Halmashauri huwa inapata miradi hii baada ya kukizi vigezo mbalimbali vya ukusanyaji wa mapato na uendeshaji wa Halamshauri kwa uwazi na ushitikishwaji wa wananchi katika kupanga na kuibua miradi ya maendeleo.
Alisema kati ya fedha hizo, Sh. Bilioni 24,382,290,527.72 zimetokana na Mradi huo wa ULGSP na Sh. Bilioni 5,434,705,202.7 zimetokana na Mfuko wa Barabara.
Aidha katika taarifa yake, Mwandezi alisema kwa mwaka wa fedha 2018/2019, serikali imetenga fedha Sh. Bilioni 2,715,890,000 kutoka Mfuko wa Barabara kwa ajili ya matengenezo ya barabara na madaraja kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
Kwa mujibu wa Mwandezi, Manispaa ya Moshi kwa sasa inaendelea na ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 0.4 ambazo zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Alisema pamoja na miradi hiyo ya barabara, pia, Manispaa hiyo imeshapokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa dampo la kisasa, ambalo ujenzi wake unatarajiwa kuanza rasmi mwezi Septemba mwaka huu, baada ya kukamilika kwa kazi ya kuandaa michoro na kupata cheti cha mazingira.
Kutokana na mafanikio hayo, serikali imeitengea tena Manispaa ya Moshi kiasi cha Sh. Bilioni 2,373,026,999 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa dampo, uwekaji taa za barabarani na ujenzi wa barabara kupitia mradi wa ULGSP.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi