Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imesaini mkataba na kampuni ya ukandarasi ya kimataifa ya CRJE (EAST AFRICA LTD), kwa ajili ujenzi wa kituo cha Kimataifa cha mabasi cha Ngangamfumuni.
Ujenzi wa kituo hiki cha Kimataifa cha mabasi cha Ngangamfumuni(Ngangamfuni International Bus Stand Terminal ) utaanza rasmi Januari 17 mwaka huu mbapo hadi kukamilika mradi huu wa ujenzi utagharimu zaidi ya tsh bilioni 27.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi wa Manispaa ya
Moshi, Michael Mwandezi alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho utatekelezwa kwa awamu tatu tofauti huku ukichukua muda wa miaka miwili hadi kukamilika.
Hata hivyo Mwandezi alisema kuwa mradi huo mpya wa kituo cha mabasi utaibadilisha Manispaa hiyo katika Nyanja ya kichumi pamoja na utekelekezaji wa malengo ya Serikali kuhakikisha miradi yake inakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Moshi Rayamod Mboya alisema kuwa,ujenzi wa kituo cha Ngangamfumuni ulisubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa Manispaa ya Moshi na wadau wa usafirishaji hivyo kukamilika kwake kutaongeza hadhi pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi.
Alisema ujenzi wa kituo hicho cha mabasi utatekelezwa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni kukamilisha eneo la maegesho ili kuweza kuanza kazi ambapo awamu nyingine ni pamoja na kuanza ujenzi wa jengo la gorofa tano ambalo litakuwa na Hoteli,maduka, migahawa pamoja na ofisi mbalimbali.
Kukamilika kwa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha ngangamfumuni kutaifanya Manispaa ya kuwa mojawapo ya Manispaa zitakazokuwa na kituo ya mabasi chenye ubora zaidi nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi