Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imesaini mkataba na kampuni ya ukandarasi ya Rocktrotinic Ltd. ya Mjini Moshi kwa ajili ukarabati na uboreshaji wa dampo la kutupia taka ngumu utakaogharimu kiasi tsh billion 2.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mkuu wa Idara ya usafi na Mazingira Danford Kamenya alisema kuwa uboreshaji wa dampo hilo utafanyika katika eneo la Mtakuja na uboreshaji huo utakuwa ni kujenga eneo na kuzikia taka ngumu,kujenga uzio na kujenga ofisi ya Meneja wa Dampo.
Hata hivyo Kamenya alisema kuwa mradi huo wa uboreshaji wa dampo utafanyika kwa muda wa miezi sita na utasaidia utupaji wa taka ngumu kwa njia ya kisasa kwa taka hizo zitakuwa zikiwekwa kwenye shimo hilo na kisha kufukiwa kwa udongo na kushindiliwa mara kwa mara.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi Rayamod Mboya alisema kuwa uboreshaji wa dampo hilo utasaidia kuboresha usafi wa mazingira katika manispaa ya Moshi kwani kwa muda mrefu dampo hilo lilikuwa katika hali isiyoridhisha kabisa.
“Tanategemea uboreshaji wa dampo hili utasaidia sana Manispaa kuendelea kuongoza katika usafi wa mazingira kwani sasa itakuwa inatupa taka zake kwenye sehemu inayokidhi viwango vya usafi na utunzaji wa Mazingira.”Alisema Meya Mboya.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi