Moshi.Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro,imeandikisha wanafunzi 3,577, wa darasa la kwanza, sawa na asilimia 101,ya lengo lililokuwa limewekwa.
Wakati darasa la kwanza wakiandikishwa hao, darasa la awali wameandikishwa wanafunzi 2,435, sawa na asilimia 80 ya lengo.
Akitoa taarifa ya uandikishaji wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2018, Mkuu wa idara ya Elimu ya Msingi Manispaa ya Moshi, Patrick Leyana, alisema katika uandikishaji huo,darasa la kwanza, wavulana ni 1,821 huku wasichana wakiwa 1,756.
Alisema zoezi la uandikishaji litamalizika Marchi 31,mwaka huu,na kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao shule,kuanzia darasa la awali,ili kuwajengea uelewa na kuwapa urahisi watakapojiunga na Darasa la kwanza.
Katika hatua nyingine Leyana alisema,Manispaa hiyo inakabiliwa na upugufu wa walimu zaidi 102,wa shule za msingi,huku zaidi ya walimu 35, wakitarajiwa kustaafu katika kipindi cha mwaka 2018,hali ambayo itaongeza upungufu huo.
Alisema mahitaji ya walimu katika Manispaa hiyo ni 742, lakini waliopo ni 640, na kupelekea kuwepo pungufu ya waalimu 102.
Wakizungunza baadhi ya walimu wa shule za msingi,walisema kumekuwepo na wazazi wachache ambao hawapeleki watoto wao madarasa ya awali,hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu walimu wa darasa la Kwanza.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi