Halmashauri ya Manispaa ya Moshi , imenunua Kijiko(Excavotor)kwa ajili ya kufanya kazi za kushindilia na kusambaza taka ngumu katika Dampo lake kuhakikisha linakuwa katika hali ya ubora na kuboresha shughuli za usafi wa mazingira ili kuiwezesha manispaa kuendelea kung’ara kiusafi ,Kitaifa na kimataifa.
Manispaa Moshi huzalisha tani 230 za takataka kwa siku, na kwa sasa ipo katika mpango wa kujenga dampo la kisasa kwa kutumia fedha za benki ya Dunia.Vile vile katika mwaka huu wa fedha Manispaa ya Moshi inatarajia kununua magari matatu mapya ya taka hivyo kuongeza idadi ya magari ya kuzolea taka kutoka Matano yaliyopo sasa hadi kufikia Nane.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Excavator hiyo, Mkuu wa idara ya usafi na Mazingira Danford Kamenya, alisema tumenunua kijiko hicho kwa Shilingi 300milion kutoka katika mapato yao ya ndani na kwamba kitasaidia kuboresha maeneo ya Dampo na kuwezesha kanuni za afya na usafi wa mazingira kuzingatiwa.
“Halmashauri imenunua mtambo huu mahususi katika kuhakikisha Dampo linakauwa katika hali nzuri na kazi hii itakuwa endelevu, kwani tumepata changamoto kubwa wakati wa mvua,na tuna mkakati mkubwa wa kuboresha shughuli za udhibiti wa taka ngumu kwa kuongeza idadi ya magari kutoka matano yaliyopo kwa sasa hadi kufikia nane”alisema
Kamenya.
Alisema magari watakayonunuliwa yatagharimu shilingi 600milion,na yataongeza uwezo wa uzoaji taka kutoka Tani 168 zinazozolewa kwa siku hadi kufikia tani 230, na kufanya mji kuendelea kuwa katika hali ya usafi wakati wote.
Akizungumzia ujenzi wa Dampo mpya, Kamenya alisema,katika eneo ambalo tutajenga Dampo pia tanatarajia kujenga kiwanda cha kuchakata
takataka na kuzalisha mbolea ambacho k
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi