Mwajabu Iddi Songwe (55), ni mkazi wa Mtaa wa Sokoni Kata ya Bomambuzi, ambaye anaishi na wajukuu watano, ambapo wanne wanasoma shule ya msingi huku mmoja akisoma shule ya msingi.
Bi mwajabu ni mnufaika wa mradi wa TASAF ambapo anapokea tsh 72,000 ambayo imemuwezesha kuwasomesha wajukuu zake watano kwa kuwalipia ada kwani walikuwa ni tegemezi kwake.
“Kabla ya kuingia kwenye mradi huu wa TASAF nilipitia katika kipindi kigumu kuweza kuwalipia wajukuu zangu ada pamoja na sare za shule, lakini fedha ambazo nimekuwa nikizipata zimekuwa msaada mkubwa kwa wajukuu zangu kuweza kupata elimu na kupunguza ugumu wa maisha”Anaeleza Bi Mwajabu.
Anasema Fedha hizo hakuishia kulipa ada pekee pia amejiunga kwenye vikoba na pia amefungua biashara ya genge ambayo anauza samaki, na nyanya,hoho na karoti na vitunguu ambayo inamuewesha kupata fedha ya kuhudumia familia.
“Matarajio yangu ni kukopa na kukuza zaidi biashara yangu ya genge ili kuwa na mtaji mkubwa na kuuza bidhaa mbalmbali ambayo itaniwezesha kupata fedha za kununua kiwanja kwa ajili ya kujenga nyumba kwani kwa sasa naishi kwenye nyumba ya kupanga hivyo nalazimika kulipa kodi”Anasema Mwajuma.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi