“Nilianza kwa kufuga bata wadogo baada ya walikua niliwauza na kupata fedha ya kuanzisha miradi midogo midogo na nilijiunga kwenye vikundi ambavyo viliniwezesha kukopa na kuanza kununua vifaa vya ujenzi na kwa sasa nimekamilisha ujenzi wa nyumba ya kuishi”.
Hayo yanabainishwa na Amina Mruma mmoja wa wanufaika wa TASAF kutoka Mtaa wa Matindigani Kata ya Pasua.
Amina anapokea kiasi cha Tsh 72,000 kwenye zoezi la uhawilishaji fedha kila baada ya miezi miwili kiasi ambacho ameweza kukitumia kuanzisha miradi midogo midogo,kusomesha watoto na hatimae kujenga nyumba ya kuishi.
Anasema alianza kwa kununua bata wadogo wa tsh 30,000 na baadae walikuwa na kuuza na kupata tsh 100,000 ambazo pia alizitumia kama hisa kwenye vikoba iliyomuwezesha kukopa na kununa vifaa vya ujenzi.
“Kupitia mradi wa ufugaji wa bata na biashara ya genge pamoja na kukopa nilianza kununua vifaa vya ujenzi kwa awamu hadi kuweza kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya vyumba viwili ambayo hata hivyo mpango wangu ni kuendelea na ujenzi kuwa na makazo bota”Anasema Amina.
Akielezea maisha yake kabla ya kuingia kwenye mradi wa TASAF, Amina anasema maisha yalikuwa magumu na kushindwa kumuda mlo mmoja kwa siku, huku wakiishi makazi duni,na kushindwa kulipa ada na kununua sare za shule.
“Naweza kusema TASAF imebadilisha maisha yangu kwani mambo yote nimeweza kuyafanya kupitia fedha ambazo nlikuwa nazipata ikiwemo kulipa ada na sare za watoto pamoja na kuendelea na miradi midogo midogo”.
Amina anamtizamo tofauti na wanufaika wanaosema fedha wanazopewa na TASAF ni kidogo, anasema hakuna fedha ndogo inategemea na jinsi watu wanavyofikiri pamoja na matumizi sahihi ya fedha.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi