SERIKALI yaahidi kutoa kiasi ya Tsh. Bilion 10 kwa ajili ya kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Stand mpya ya kimataifa ya Ngangamfumuni Manispaa ya Moshi.
Hayo yalielezwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha mabasi katika eneo la Ngangamfumuni wakati akizungumza wananchi akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika mkoa wa Kilimanjaro ,
Alieleza mradi huu ni wa kimkakati kwani mkoa wa Kilimanjaro upo mpakani hivyo uwepo wa kituo cha mabasi cha kisasa utatoa fursa kwa wakazi wa mkoa huu kufanya biashara kwa kuwa utapokea mabasi kutoka nchi za jirani ikiwemo Kenya.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi