Mkuu wa Wilaya ya Moshi Saidi Mtanda ameeleza kuwa sababu zinazosababisha Serikali kuu kuingilia maamuzi ambayo yamekuwa yakifanywa na baraza la madiwani ni pamoja na uwepo wa maamuzi ya baraza la madiwani yasiyofuata Katiba, Sera za Kitaifa,Sheria, Kanuni na miongozo inayotolewa na Serikali.
Mtanda ametoa kauli hiyo wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa idara wa Manispaa ya Moshi kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji ikiwemo misingi ya maadili ya viongozi wa umma, majukumu ya waheshimiwa madiwani, usimamizi wa Rasilimali fedha katika serikali za mitaa,Mahusiano ya madiwani na watendaji na uhusiano kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
“Sisi tunapojiridhisha kwamba baraza linatekeleza wajibu wake kwa kufuata Katiba ya Nchi, Sheria, na kanuni na kufuata huwa hatuna maneno na nyie lakini baraza mkifanya maamuzi kinyume na utaratibu huwa tunatoa maelezo na ushauri wa namna ya kufanya ili mambo yaenda sawasawa”Alisema Mtanda.
Mtanda alisisitiza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ipo tayari wakati wowote kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani na Serikali kuu huwa haina tabia ya kuingilia maamuzi ya baraza la madiwani bali kinachofanyika ni kushauri ili kuhakikisha kunakuwepo na utawala bora unaofuta sheria za nchi.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Juma Raibu amesema mafunzo hayo yatawawezesha madiwani na watendaji kushirikianza kwa karibu katika kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kuwaletea wananchi wa Manispaa ya Moshi Maendeleo.
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya sisi Madiwani wa Manispaa ya Moshi tunashirikiana vizuri na Watendaji na hakuna mgogoro wowote kwani tunafanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimiana “.Alisema Raibu.
Mstahiki Meya ameeleza kuwa mafunzo haya yatakuwa chachu kwao katika kuendesha Halmashauri kwani kwa sasa Waheshimiwa madiwani wameongeza elimu kwa kujua majukumu yao hasa katika kusimamia Rasimali fedha na mahusiano kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi