Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Mh. Juma Raibu ameahidi kutoa donge nono kwa Mwananchi yeyote atakayefichua au kusaidia kukamatwa kwa wahalifu wanaoharibu na wanaoiba nyaya na betri za taa za barabarani zinazotumia umeme wa jua(Solor) kwenye barabara za manispaa ya Moshi.
Akizungumza katika kikao cha kwanza cha baraza la madiwani Mstahiki Meya alisema kuna baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya Manispaa ya Moshi wamekuwa wakihujumu miundo mbinu ya taa za barabarani hasa kwenye barabara ya Sukari, Bonite na barabara ya Tembo iliyopo kata ya Bomambuzi.
“Tunaomba sana vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na Madiwani wetu kuhakikisha wale wote wanaoharibu na kuiba miundo mbinu ya taa za barabarani wakamatwe haraka na kufunguliwa kesi za hujumu uchumi kwani serikani imetoa fedha nyingi kugharamia miundo mbinu hii kwa manufaa ya wakazi wa Manispaa ya Moshi”Alisema Mh. Juma Raibu
Mstahiki Meya aliongeza kuwa katika uongozi wake atapambana usiku na mchana na kikundi hicho cha watu kinachoiba miundo mbinu ya taa za barabarani kisichokuwa nia njema kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi .Mradi huu wa taa za barabarani umekuwa na mchango mkubwa katika usalama wa wananchi kwa kupunguza uhalifu hasa nyakati za usiku hivyo anawataka wahalifu hao kuacha tabia hiyo mara moja .
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi