Halmashauri ya manispaa ya moshi imekabidhi pikipiki 21 kwa waratibu wa elimu wa kata 21 za manispaa ya Moshi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu na kuwataka waratibu hao kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Pikipiki hizo zimekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kipi Warioba leo tarehe 4 septemba katika Bohari ya manispaa ya Moshi kwa lengo la kuwasaidia waratibu wa elimu katika kuendesha na kuratibu shughuli za kielimu.
Akizungumza kabla ya kukabidhi pikipiki hizo alisema kuwa anauzoefu na baadhi ya watendaji kupewa vitendea kazi na serikali hasa pikipiki kuziweka nyumbani na kuzifanyia bodaboda badala ya kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Nawataka waratibu wote kutumia pikipiki hizi kwa ajili ya kuboresha elimu kwa kukagua shule zetu na kufuatilia maendeledo ya elimu katika shule zetu za msingi na sekondari” alisema Warioba.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya moshi Ndg. Michael Mwandezi alisema hizi pikipiki zimetolewa na serikali ya awamu ya tano ili kuhakikisha kuwa elimu inaboreshwa kwa wanafunzi wote wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu(KKK).
“Serikali ya awamu ya tano imeamuwa kuweka nguvu nyingi kwaajili ya ufatiliaji na uratibu wa shughuli zote za kielimu ndio maana imeboresha utendaji kazi kwa kuwapatia vifaa”Alisema Mwandezi
Akishukuru kwa niaba ya waratibu wa elimu kata mratibu wa elimu Kata ya Miembeni Mwl.Godfrey Shirima aliipongeza serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapatia pikipiki hizo.
“Tunakuhakikishia Mh Mkuu wa Wilaya kuwa tutazitumia pikipiki hizi vizuri kwa shughuli za kielimu na tuhahidi kuwa ufaulu utaongezeka katika manispaa ya Moshi na kuwa ya kwanza kitaifa katika matokeo ya darasa la saba”. Alisema Shirima.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi