Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi, Mh. Juma Raibu Juma,ameahidi kushirikiana na Madiwani wote pamoja na Watendaji wa Halmashauri katika kufanya kazi kwa bidii , weledi na kuzingatia maadili ili kuharakisha Maendeleo ya Manispaa ya Moshi na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025..
Akizungumza katika kikao maalumu cha Baraza la madiwani mara baada ya kuchaguliwa kuwa Meya kwa ushindi wa asilimia Mia Moja , Mh. Juma, alisema madiwani na watendaji kwa pamoja wanawajibu mkubwa wa kushirikiana kuwatetea wanyonge na kuwaletea wananchi wa Manispaa ya Moshi maendeleo.
“Leo tumeapishwa na kuwa madiwani na tukumbuke kuwa kwa kiapo hiki tunalo deni kubwa kwa wananchi na wajibu wetu kama viongozi tukishirikiana na watendaji ni kutatua kero za wakazi wa Manispaa ya Moshi hasa wanyonge I kama alivyoahidi Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli wakati wa kampeni.”alisema Mstahiki Meya
Aidha Mstahiki Meya alisema Halmashauri imedhamiria kuhakikisha inakuharakisha kutukeleza vigezo vya kuwa Jiji ili mchakato wa Kupandisha hadhi Manispaa ya Moshi na kuwa jiji unamalizika haraka hatua ambayo itasaidia kukuza uchumi na kuwaletea wananchi wa Moshi maendeleo wanayotarajia.
Alisema vipaumbele vingine vya Halmashauri ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara hasa za pembezoni,kuwatengea wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanyia biashara, kuboresha sekta Afya kwa kujenga Hospitali ya Wilaya , kuongeza ufaulu katika elimu na kufufua michezo na kukuza vipaji.
“Tunavyo vipaumbele vingi vya kutekeleza katika kipindi hiki cha miaka mitano kwa ajili ya kuwaletea wakazi wetu maendeleo na nitahakikisha kwa kushirikana na Mh Mbunge wetu tunatafuta wawekezaji wa kuwekeza kwenye viwanda vipya na kufufua viwanda vilivyokufa.”alisema
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Michael Mwandezi, alisema atahakikisha anatoa ushirikiano wa kutosha kwa madiwani ikiwa pamoja na kusimamia sheria, kanuni na taratibu katika masuala mbalimbali kwa lengo la kuharakisha maendeleo kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi.
“Hongereni kwa kuchaguliwa kuwaongoza wananchi wa Manispaa ya Moshi na nina waahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa kuzingatia sheria , kanuni, maadili na miongozo mbalimbali ili kufikia malengo ya kuisadia Manispaa ya Moshi kupiga hatua zaidi katika maendeleo”alisema Mwandezi
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi