Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imetoa mikopo yenye thamani ya tsh Milioni 200 kwa vikundi 40 vya wanawake na vijana pamoja na walemavu ikiwa ni utekeleza wa agizo la serikali la ya Awamu ya Tano ya Rais Mh. Dr. John Pombe Magufuli la kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Wanawake,Vijana na Walemavu.
Akikabidhi mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba amewataka kinamama, vijana pamoja na walemavu kuzitumia fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa na kuhakikisha wanarejesha mikopo hiyo ili Halmashauri iweze kukopesha vikundi vingine.
Warioba amewataka wajasiriamali waliokopeshwa fedha hizo kurejesha kulingana na taratibu walizowekewa ili kuweza kuitumia fursa hiyo kukopa kwa awamu nyingine na kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwao pamoja na Taifa kwa ujumla.
Awali, Mkuu wa Idara Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii Bi. Rose Minja alisema kutolewa kwa mikopo hiyo kunaifanya manispaa ya moshi iwe imetoa mikopo ya jumla ya shs.534mi/= kwa vikundi 104 kwa miaka miwili baada ya mwaka jana kutoa mkopo wa shs. 334mil/= kwa vikundi 64.
“Mpaka sasa vikundi ambavyo tumevipatia mikopo vinarejesha kwa asilia kubwa ambapo licha ya uhamasishaji tunaofanya bado kuna idadi ndogo ya vijana na walemavu wanaojitokeza kwa ajili ya kuomba mikopo hiyo”Alisema Rose.
Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Moshi Raymond Mboya alitoa wito kuwa utoawaji wa mikopo hii ufuate vigezo vilivyowekwa na kuwaomba watendaji kutoingiza siasa na aliwataka wananchi kuweka tofauti za vyama pembeni na kuwa na umoja katika kufikia malengo mbalimbali ya kiuchumi waliyojiwekea.
Dafrosa Kimaro ambaye ni mjasiriamali kutoka kikundi cha Kirashi kilichopo Kata ya Longuo B ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajali na kuwapatia mikopo makundi yenye uhitaji maalumu kwani itawainua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi