Imeelezwa kuwa,Mila kandamizi na mfumo dume uliopo katika jamii, ni changamoto inayowanyima wanawake fursa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kumiliki mali ikiwemo Ardhi.
Mbali na hilo,vitendo vya kikatili, vinavyoendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali nchini,pia vimekuwa vikiwakandamiza wanawake katika kupata haki na kuwafanya kudharaulika katika jamii.
Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Miradi katika asasi isiyo ya kiserikali ya Elimu Mwangaza Tanzania, Upendo Ramadhani,wakati akisoma taarifa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, katika Manispaa ya Moshi .
Upendo alisema,pamoja na mafanikio ambayo wameyapata wanawake,bado wanakumbana na vikwazo mbalimbali ikiwemo mila na desturi kandamizi ambazo zinawanyima fursa ya kuwa viongozi katika ngazi za kutoa maamuzi, kwenye familia na hata kwenye jamii.
"Mila,Desturi na mfumo dume,bado ni changamoto kwa wanawake katika jamii nyingi nchini, na changamoto hii inawanyima wanawake haki ya kuzungumza kutoa maoni,kuwa viongozi na kumiliki mali ikiwemo Ardhi"alisema.
Katika hatua nyingine, alisema pamoja na serikali kufanya kazi nzuri kusaidia wanawake,bado kuna urasimu wa sera na mifumo isiyo rafiki kwa wajasiriamali wadogo.
Akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,Danford Kamenya, alisema katika kipindi cha mwaka 2016/17 Manispaa hiyo imetoa Sh.234milioni,kwa vikundi vya wanawake 53,ikiwa ni hatua mojawapo ya kuwawezesha kiuchumi.
Alisema katika kupindi cha mwaka 2017/2018, imetolewa Sh. 195Milion, kwa vikundi 39 na kwamba fedha hizo zimewawezesha wanawake kuanzisha shughuli za ujasiriamali na kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi Mh.Peter Minja,alisema soko limekuwa tatizo kwa wajasiriamali wengi na kushauri wajasiriamali kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kuweza kuingia kwenye ushindani.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi