Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa kipindi cha Mwezi Machi,2021 hadi Oktoba 2023 imefanikiwa kutoa mikopo isiyo na riba yenye Jumla Tshs. 2,581,481,990 kwa vikundi 417 ikiwa ni utekeleza wa agizo la serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Dr Samia Suluhu Hassan la kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Wanawake,Vijana na Watu Wenye Walemavu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Rashid Gembe ameeleza kuwa hii ni ongezeko la Tshs 748,761,295 na mikopo hiyo imetolewa kwa vikundi vya wajasiriamali mbalimbali kwenye Kata 21 za Manispaa ya Moshi ambapo Vikundi 295 vya wanawake vimepata Shs 1,682,759,802 vikundi 100 vya vijana vimepewa Ths 846,824,188 na vikundi 22 vya Watu Wenye Ulemavu vimepata kiasi cha Ths 57,899,000.
“Kumekuwepo na mwitikio mkubwa kwa makundi yote ukiacha kundi moja la Watu Wenye Ulemavu,ambapo tumekuwa tukisisitiza kujikita katika kuanzisha miradi yenye tija ili kuweza kupata matokeo chanya kwenye uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa”Alisema Gembe
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi