Halamshauri ya Manispaa ya Moshi imetoa Mikopo isiyo na riba ya Tsh . 357,573,000/= kwa Vikundi 18 vya Wanawake na Vijana ambapo Vikundi 9 vya Wanawake vimepewa Tsh. 97,600,000/= na Vikundi vya Vijana 9 vimepewa Tsh. 259,973,000/=.
Akizungumza Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe amesema wamekabidhi fedha na vyombo vya moto (Bajaji na Bodaboda) vyenye thamani ya Tsh. 357,573,000/= kwa vikundi hivyo kutokana na kukidhi vigezo vilivyowekwa.
Nasombe alisema toka lifunguliwe dirisha la utoaji wa Mikopo na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Novemba 2024 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imefanikiwa kutoa mikopo ya Shilingi Bilioni 1.1 ambapo kiasi cha shilingi milioni 800 zilizotolewa kwa awamu ya kwanza mwishoni wa mwezi Novemba 2024.
Aidha amewataka wanufaika hao kuitumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusidiwa na kuhakikisha kuwa waaminifu kwa matumizi ya fedha hizo na kuhakikisha wanazirijesha kwa wakati ili ziweze kunufaisha walengwa wengine. walivyoomba.
Naye, Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi Mhe. Stuart Nkinda amewataka wanufaika hao kurejesha mikopo hiyo kwa wakati kwani kufanya hivyo itawasaidia wananchi wengine kukopa na kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kwa ajili ya maendeleo yao na Manispaa kwa ujumla.
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa mkopo hiyo Ally Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi Cha Quality Printind ametoa shukrana na kupongeza mfumo mpya wa utoaji mikopo ulioanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kuahidi kuwa watatumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanarejesha kwa wakati.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi