Halmashauri ya manispaa ya Moshi,imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 295 kwa vikundi 44 vikiwemo vikundi 31 vya wanawake,11 vya vijana na vikundi 2 kwa watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwaongezea mitaji wajasiriamali na kukuza uchumi wao kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na mkuu wa Idara Maendeleo ya Jamii Rose Minja, wakati wa hafla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Ths 295,955,000/= iliyofanyika katika Viwanja vya ofisi ya Kata Majengo ikiwa ni gawio la robo ya kwanza la asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022.
Minja alisema vikundi vilivyopewa mikopo hii isiyo na riba vinajishughulisha na uanzishaji wa viwanda vidogo kama vile ushonaji wa nguo, utengenezaji wa batiki,utengenezaji wa sabuni,utengezaji wa mvinyo na kufanya biashara ndogo ndogo.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Juma Raibu aliwataka wanufaika wa mikopo hiyo kuhakikisha kuwa fedha wanazopewa zinakwenda kutekeleza miradi /biashara walizokusudia na wajenge tabia ya kuzirejesha kwa wakati ili ziweze kunufaisha vikundi vingi zaidi kama inavyotarajiwa.
“Baadhi yenu mmekuwa mkipata mikopo hii mnaifanyia shughuli nyingine zisizo na tija badala kuwekeza kwenye biashara na miradi iliyokusudiwa na kusababisha kuleta usumbufu wakati wa Marejesho.Nasema hapa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi haitamvumulia mtu yoyote atakeyechezea fedha hizi na wale wote watakaoleta udanganyifu tutawakamata na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.Nyinyi leo mnanufaika na mikopo hii isiyo na riba inayotolewa na serikali mnayo nafasi kubwa ya kujikwamua kiuchumi na kuzisaidia familia zenu” Alisema Mstahiki Meya Raibu
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi