BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi limepitisha rasimu ya Sheria Ndogo ya kuruhusu ukarabati wa Majengo kwenye maeneo ya biashara yaliyo katikati ya Mji (Central Business District).
Rasimu hiyo ya Sheria ya ukarabati ina lengo la kuweka uwazi wa jinsi ya kupata kibali cha ukarabati na kuondoa urasimu uliokuwepo hapo awali.
Akizungumza baada ya kupitishwa kwa rasimu hiyo Meya wa Manaispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi Kidumo alisema sheria hii itasawasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kujenga ghorofa waweze kukarabati majengo yao ili yawe katika hali nzuri inayoendana na hadhi ya Manispaa ya Moshi.
“Sio siri kuna baadhi ya nyumba zilizopo katika ya Mji ni chakavu na wanaoishi kwenye nyumba hizo kwa sasa hawana uwezo wa kujenga ghorofa hivyo Halmashauri imeona kuna umuhimu wa kupitisha sheria hii ili kuwasaidia waweze kufanya ukarabati na kukaa mahali pazuri na salama”Alisema Mhandisi Zuberi
Sheria hii pia itasaidia Manispaa ya Moshi kuongeza mapato kwani kuna viwango mbalimbali vimewekwa kama ada ya kibali cha ukarabati mjini.
Naye Mwanasheria wa Manispaa ya Manispaa ya Moshi,Sifael Kulanga alisema rasimu hii ya Sheria ndogo ni ya ukarabati wa Majengo katika ya Mji na haijafuta Sheria na utaratibu wa maombi vibali vya ujenzi wala Mpango Kabambe (Master Plan) unaomtaka mmiliki wa kiwanja/jengo katikati ya Mji hasa Kata za Bondeni,Mawenzi , Kiusa na baadhi ya maeneo la Kata ya Korongoni kama mtu anataka kujenga ajenge jengo la ghorofa.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi