Baraza la Madiwani la Manispaa ya Moshi, limepitisha bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/202 ambayo ni zaidi ya Sh. Bilioni . 52,543,437,312.00
Mstahiki Meya wa Manispaa Juma Raibu Juma, alitangaza bajeti hiyo , wakati akifunga kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili na kuidhinisha mapendekezo ya bajeti.
“Bajeti hii ya Shilingi billion 52,543,437,312.00 tuliyoipitisha leo, inajumuisha miradi ya maendeleo, mishahara na matumizi mengineyo ya Manispaa yetu, lakini mapato ya ndani ni sh. bilioni 6,432, 335,672 na hii ni pamoja na ongezeko la zaidi shilingi milioni 150,”alisema Mstahiki Meya
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imeweza kupandisha mapato yake kutoka kwenye vyanzo vyake kutoka kiasi cha sh. bilioni 6.2 hadi kufikia 6.4.
Kutokana na mafanikio hayo, Mstahiki Meya huyo alimwomba Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Bw. Uhuru Mwembe kuhakikisha kuwa anasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ili bajeti hiyo iweze kufikiwa kwa lengo la kuwaletea wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Maendeleo .
.Aidha Mstahiki Meya alisema Manispaa imejipanga kuhakikisha inaweka nguvu zake katika ukusanyaji mapato na kusimamia miradi miradi ya maendeleo ili ilete mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi na wakazi wa Manispaa ya Moshi .
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi