Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mh. Kippi Warioba amewataka washiriki wa kikako kazi cha kujadili Mpango Kabambe wa Manispaa ya Moshi wa Mwaka 2019-2039 kuzingatia mahitaji ya wananchi wanapojadili ili mpango uweze kuwarahisishia wananchi katika shughuli zao maendeleo.
Akifungua kikao kazi cha kujadili Mpango Kabambe katika ukumbi Mkuu wa Mkoa 19 Decemba 2019 ,Warioba amesema kuwa suala la ukuaji wa mji huwa haliepukiki hivyo changamoto zote zinazotokana na ukuaji wa mji zitumike kama fursa na kuhakikisha zinawekwa katika Mpango Kabambe ambao ndio dira na muelekeo wetu kwa miaka ijayo.
Alisema suala kubwa katika Mpango Kabambe ni kujua shughuli zote za kijamii,Kiuchumi,Kiutawala na kimazingira zinafanyika juu ya ardhi,hivyo ni muhimu kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kutumia rasilimali ardhi ili kutumia rasilimali ardhi kwa ufanisi na kuleta maendeleo endelevu.
“Ni matumaini yangu kuwa mpango huu utakapokamilika tutahakikisha kuwa tunautekeleza ili uweze kusimamia na kuratibu shughuli zote za maendeleo na ukuaji wa Manispaa yetu”Warioba alisema
Aidha ifahamike kuwa Manispaa ya Moshi ndipo yaliyopo Makao Makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro ambapo shughuli zote za kiutawala,kijamii na kiuchumi zinafanyika,Kwahiyo mji huu ni kitovu cha utawala na ukuaji wa uchumi Mkoa wa Kilimanjaro,Kwa undaa kuutekeleza na kuusimamia huu Mpango Kabambe,mji huu utakuwa kwa utaratibu mzuri kwa vile utakuwa na meaneo ya wazi,maeneo ya makazi,viwanda,huduma za jamii,biashara,taasisi na sehemu za starehe na michezo.
“Mpango wa huu Kabambe utatoa fursa ya idadi kubwa ya watu hasa vijana kutoka vijijini kujitafutia riziki na kwa kuuza bidhaa mbalimbali”Alisema.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi