Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi Tsh Bilioni 1.8 kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 ya utawala wa Rais wa awamu ya 5 Dr. John Joseph Magufuli kwa lengo la kuinua kipato cha wananchi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara Maendeleo ya jamii Manispaa ya Moshi, Rose Njau wakati wa utoaji wa mikopo kwa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo Halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya Tsh milioni 281 kwa vikundi vya wanawake na Vijana.
“Kumekuwepo na mwitikio mkubwa kwa makundi yote ukiacha kundi moja la watu wenye ulemavu,ambapo tumekuwa tukisisitiza kujikita katika kuanzisha miradi yenye tija ili kuweza kupata matokeo chanya kwenye uchumi wa wananchi na taifa”Alisema Rose Minja
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mwanasheria wa Manispaa ya Moshi Iddi Ndabhona alisema mafanikio makubwa yameonekana kutokana na mikopo isiyokuwa na riba kwa vikundi wajasiriamali hivyo kwasasa wajasiriamali wanapaswa kujikita kuanzisha viwanda vidogo ili kuleta matokeo chanya kwenye uchumi wa viwanda.
“Leo tumetoa mkopo kwa vikundi vya wanawake 30 wenye thamani ya Tsh Milioni 172,vikundi 12 vya vijana milioni Tsh. 109, ambapo kwa awamu hii hatujafanikiwa kupata maombi ya vikundi vya watu wenyeulemavu hivyo Halmashauri inaendelea kuhamasisha na kusisitiza walemavu wajitokeze kwa ajili ya kupata mikopo hii isiyokuwa na riba”Alisema. Idd Ndabhona
Nao wanavikundi wanaeleza kuwa mikopo inayotolewa na Halmashauri ambayo haina riba imekuwa na mchango mkubwa kwenye miradi yao, pamoja na kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na kuchangia pato la taifa.
Kwa mujibu wa sheria ya usimamizi na utoaji wa mikopo ya mwaka 2019 halmshauri zote nchini zinapaswa kutenga asilimia 10 ya mapato yake ili kuwezesha vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi