Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imefanikiwa kutoa mikopo isiyo riba kwa asilimia 100 yenye thamani ya tsh Milioni 690,324,000 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa ni utekeleza wa agizo la serikali la ya Awamu ya Tano ya Rais Mh. Dr. John Pombe Magufuli la kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Wanawake,Vijana na Walemavu.
Mikopo hiyo imetolewa kwa vikundi vya wajasiriamali mbalimbali kutoka katika kata 21 za Manispaa ya Moshi ambapo Vikundi 65 vya wanawake vimepata Ths 413,000,000,Vikundi vya vijana 33 vimepewa Ths 257,302,000 na vikundi vya watu wenye ulemavu 4 vimepata kiasi cha Ths 20,000,000.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi