UJUMBE wa watu watano kutoka mji wa Suncheon nchini Korea Kusini ukiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Mr.Choong-Hoon Cho wametembelea manispaa ya Moshi na kusaini makubaliano ya kiungwana na Halmshauri ya Manispaa ya Moshi kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika masuala ya Sayansi na Teknolojia.Mbali na hilo pia wamekubaliana kushirikiana na kubadililishanauzoefu katika sekta ya Elimu,utamaduni pamoja na kubadilishana wa jinsi ya kutunza taka ngumu na utunzaji wa Mazingira.
Akizungumza Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Michael Mwandezi alisema kuwa, ujio wa Meya huyo wa korea na wajumbe wake unatokana na juhudi za serikali kuboresha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali Duniani.
"Kama unavyojua, serikali ya Tanzania imefungua Ubalozi wakeKorea ya Kusini mwaka huu, na hii imefungua milango ya kibiashara katika nchi hizi mbili na ndio maana umeona Mstahiki Meya wa jiji Suncheon Korea amekuja na wajumbe wake kutembelea Manispaa yetu ya Moshi, hii ni fursa kubwa sana ya kutangaza bidhaa zetu na fursa za uwekezaji zilizopo Manispaa ya Moshi ..." alisema Mwandezi.
Naye Mstahiki Meya wa mji wa Suncheon nchini Korea Kusini,Choong-Hoon Cho, alitoa wito kwa serikali yaTanzania kuitangaza vyema kahawa ya Kilimanjaro kwa kuwa ina ladha ya kipekee kuliko kahawa nyingine yeyote inayolimwa Duniani.
“Kahawa ya Kilimanjaro inaonekana kuwa na ladha ya kipekee tofauti na Kahawa ambayo inatoka nchi nyingine; kwani tulipofika katika Mkoa wa Kilimanjaro hususani katika Manispaa hii tumekunywa kahawa hakika ni tofauti na nzuri kuliko ambayo tunaletewa na kunywa huko kwetu”Aliongeza“Tutakwenda kuwashawishi wafanyabiashara wa Korea ya Kusini kuja Manispaa ya Moshi kuwekeza na kuchukua kahawa ya Tanzania na kuipeleka Korea,ninatoa wito kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha inatangaza za bidhaa zao zaidi ili ziweze kujulikana kimataifa kwani inaonekana kuna bidhaa bora lakini hazijulikani hasa kwenye nchi kama niliyotoka mimi.” anafafanua Meya huyo.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya alifafanua kuwa Manispaa ya Moshi na Mji wa Suncheon wamekubalina kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo kwenye sekta ya Elimu, utamaduni, Uchumi, Mazingira pamoja na michezo.
Aidha alielezea kuwa katika ziara hii,ugeni huu umetembelea shule ya sekondari ya ufundi ya Moshi, shule Msingi ya Mwereni , shule ya Mother Theresa Daycare Centre, Chuo Kikuu cha Ushirika, Hifadhi ya mlima Kilimanjaro Kinapa na hifadhi ya taifa ya Manyara.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi