SERIKALI ya awamu ya sita imetoa jumla ya shilingi bilioni 956.63 kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo tangu Rais Dk Samia Suluhu Hassan aingie madarakani mwaka wa 2021.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw Nurdin Babu wakati wa hafla maalum ya kumbukizi ya kuzaliwa Rais Dk Samia iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Majengo ulioko Manispaa ya Moshi, mkoani humo, Jumatatu.
“Kiasi hili ni kikubwa ikilinganishwa na jumla ya shilingi milioni 285 ambazo zilishatolewa kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita; hii ni hatua kubwa kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wa Kilimanjaro”, alisema.
Bw Babu alisema kuwa kupitia fedha hizo tayari miradi 1,360 imetekelezwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo kwenye sekta za afya, elimu na miundombinu mbalimbali ikiwemo ya maji na barabara.
“Katika fedha hizo, jumla ya 117.08 bn/- zimetumika kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa taasisi za kiafya 289, pamoja na ununuzi wa dawa na vifaa tiba”, alisema na kuongeza, manispaa ya Moshi, imepokea jumla ya 3bn/- kwa ajili ha ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo alisema itakuwa ni ya ghorofa.
Aliendelea kusema kuwa katika sekta ya elimu Mkoa ulipokea jumla ya 149.64bn/- ambazo alisema zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya 1,82, shule mpya 44 zikiwemo za msingi na sekondari, ujenzi wa mabweni 106, matundu ya vyoo 305, maabara 181, shule shikizi 5, vuo vya kati pamoja va vyuo vikuu.
Aidha alisema Serikali pia imetenga fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya utalii ambayo yamechangia kuongezeka kwa watalii wanaoingia hapa nchini ikiwemo kupanda Mlima Kilimanajro ambao ndiyo mrefu kuliko yote Barani Afrika.
Bw Babu alisema kuwa kutokana na Rais Dk Samia kuwa kinara katika kuboresha na kulinda mazingira nchini, shughuli za sherehe ya kuzaliwa kwake zimeanza kwa viongozi mbalimbali wa ngazi za wilaya na Mkoa kupanda miti katika shule ya sekondari ya Lucy Lameck, iliyoko manispaa ya Moshi.
Katika hafla hiyo mbali na shughuli za kupanda mti, pia Bw Babu alikata keki maalum kwa ajili ya kuadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwa Rais Dk Samia, ikiwa ni moja wapo ya keki zilioandaliwa kwenye hafla hiyo ambazo ziligawiwa kwa waliohudhuia hafla hiyo.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi