Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiopongeza Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa usafi na ujenzi wa miundombinu.
“Nawapongeza Manispaa ya Moshi kwa usafi na ujenzi wa miuondombinu na niwataka muendelee kudumisha hali hii ya usafi na usafi uzidi zaidi”Alisema makamu wa Rais.
Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa barabara ya Bonite yenye urefu wa kilometa 2.9 iyojengwa kwa kiwango cha lami na kugharimu kiasi cha tsh. 3,169,840,303 ikiwa ni fedha kutoka serikalini.
Makamu wa Rais pamoja na kuzindua barabara ya Bonite ameweka jiwe la msingi la mradi wa upanuzi wa kituo cha afya pasua uliogharimu fedha kutoka serikalini kiasi Tsh. Milioni 400 na umekamilisha ujenzi wa majengo ya wodi ya mama na mtoto,chumba cha upasuaji,X-ray na jengo la maabara.
Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupeleka huduma bora za kimaendeleo kwa wanachi wote nchini “Alisema makamu wa Rais.
Makamu wa Rais yupo Manispaa ya Moshi katika ziara yake ya kukagua miradi na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika mkoa wa Kilimanjaro.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi