Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, imetoa
mafunzo ya sheria ya manunuzi ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya
mwaka 2016 kwa Madiwani ,hatua ambayo itawawezesha kujua dhana na msingi wa manunuzi ya umma.
Akifungua mafunzo hayo,Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi
Aisha Amour, alisema yatakuwa chachu kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo,
na kuwapa uelewa wa pamoja kati yao na watendaji, ili kusimamia
manunuzi yote yanayofanywa na Halmashauri.
Amour alisema msingi wa manunuzi ya umma, ni kuhakikisha kuwa, kuna kuwepo na
uwazi, uwajibikaji,usawa,thamani ya fedha,uadilifu na ushindani ili
kuleta bei nzuri kwa taasisi ya manunuzi, na hivyo kuwataka madiwani
kutumia mafunzo watakayoyapata kuhakikisha, sheria ya manunuzi na
marekebisho yake inafuatwa na kutekelezwa kikamilifu.
“Ndugu madiwani, Mafunzo haya mnayoyapata, ni muhimu katika
kufanikisha shughuli za manunuzi katika halmashauru yenu,na kupunguza
gharama kupitia taratibu za manunuzi, zenye ufanisi unaofaa kwa
kununua kwa usahihi ili kupata thamani ya fedha”alisema Mhandisi Amor.
Aidha alisema Madiwani wana jukumu kubwa la kusimamia Mapato na
matumizi ya halmashauri,hivyo kutolewa kwa mafunzo hayo, kufungue njia
na mwanga wa kuhakikisha michakato yote ya manunuzi katika Halmashauri
hiyo inazingatia sheria na taratibu za manunuzi.
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa Michael Mwandezi, alisema madiwani wakizingatia mada zote zitakazofundishwa, wataweza kuhakikisha Halmashauri hiyo inafanya
manunuzi kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na miongozo mbalimbali itolewayo
na Mamlaka ya usimamizi ya manunuzi ya umma.
Wakizungumza baadhi ya madiwani walioshiriki mafunzo hayo,walisema
yatakuwa chachu ya kuwawezesha kusimamia na kutekeleza sheria ya
manunuzi, ikiwa ni pamoja na kusimamia michakato yote ya manunuzi katika
Halmashauri kwa ufanisi bila upendeleo.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi