Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 umetembelea na kukagua miradi mitano yenye thamani ya zaidi ya shs bilioni 1.1 katika Manispaa ya Moshi.
Akizungumza baada ya kukagua na kutembelea miradi hiyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bw. Sahaili Geraruma,amewapongeza Uongozi na Watendaji wote waliopewa dhamana ya kusimamia miradi hiyo na kuwataka kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Mwenge wa Uhuru.
“Tumekagua na kutembea miradi yenu ni mizuri lakini tuwataka mzindae nyaraka kwa kufuata taratibu na zingatieni taaluma za watu mnapounda kamati mbalimbali za kusimamia miradi ya ujenzi”Alisema Geraruma.
Miradi iliyotembelea na kukaguliwa Manispaa ya Moshi ni uzinduzi wa madarasa mawili shule ya Sekondari Moshi,kutembea Mradi wa uwekeji wa dira za maji za malipo kabla,uwekeji wa jiwe la msingi barabara ya Lami ya Soweto- Makaburini, uwekaji jiwe la Msingi jengo la wagonjwa wanje(OPD) katika zahati ya Shirimatunda,kutembea na kituo cha Vijana cha STARJAX kinachofanya kazi za kudarizi na kupiga chapa.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi