KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024, Godfrey Eliakimu Mzava ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa kutoa zaidi ya Sh. Mil 650 za mapato ya ndani kwa ajili ya Ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Majengo. Ametoa pongezi hizo wakati alipoongoza Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 kukagua na kuweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Jukwaa la watazamaji na vyumba vya kubadilishia nguo kwa wachezaji wa mpira.
Naipongeze Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa kutenga na kutoa fedha hizi kwa ajili ya Ujenzi wa Uwanja huu pamoja na kuwa kazi hii ya ujenzi wa ipo asilimia 47 nina hakika mtaendelea kutoa hizi za mapato ya ndani kadri mnavyokusanya na mtasimia na kuhakikisha mradi huu unaisha kwa wakati. Alisema Mzava
Tumejiridhisha mradi huu pamoja na nyaraka za mradi huu baada ya kuzikagua zipo vizuri sambamba na nikiri mpaka hatua hii kazi kubwa na nzuri imefanyika.Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 tumeridhia uwekaji jiwe la msingi katika mradi huu" alisema Mzava
Akisoma taarifa ya ujenzi wa Uwanja kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Sekondari Mwl Agnes Luhwavi alisema lengo la mradi huu kuwawezesha Wananchi wa Manispaa ya Moshi na hasa Vijana kufanya Mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya zao.
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ilianzisha ujenzi wa Uwanja wa Majengo kutokana na uhitaji wa jamii kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimarisha afya zao.
Mradi huu unatarajia kukamilika tarehe 14/4/2024 na kazi zitakazotekelezwa ni ujenzi wa Uzio kuzunguka eneo la kuchezea( pitch), Ujenzi wa vyumba vya kubadilishia nguo kwa wachezaji, Ujenzi wa vyumba vya waamuzi, Ujenzi wa vyoo vya wachezaji na watazamaji na Jukwaa na Watazamaji.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi