Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kilimanjaro imeridhishwa na matumizi ya fedha kiasi cha Shilingi 750 zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ya ukarabati wa Miundombinu ya Shule kongwe ya Sekondari ya Mawenzi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro Jonathan Mabihya wakati wa Ziara ya Kukagua miradi iliyotekezwa na Serikali katika Halmashauri ya Manispaa ya Mosh ambapo kamati hiyo iliridhishwa na matumizi ya Shilingi Milion 500 zilizotumika kukarabati Majengo kumi na kuweza kuokoa zaidi ya Shilingi Milioni 200 ambazo zitatumika kukarabati majengo mengine ambayo hayakuwa kwenye mpango wa awali.
“Tumekagua ukarabati wa Majengo yote ya Shule hii na ninawapongeza Manispaa ya Moshi akiwemo Mstahiki Meya Juma Raibu Juma bila kusahau bodi na uongozi wa Shule kwani mmesimamia vizuri ukarabati huu na Matumizi sahihi ya fedha za Serikali yanaonekana.Hongereni sana kwani Shule imependeza sana.”Alisema Mabihya.
Aidha Uongozi wa Kamati ya Siasa ya Mkoa umeshauri Uongozi Manispaa ya Moshi kuona umuhimu wa kutenga bajeti kwa kutumia mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga bwalo la chakula kwa ajili ya wanafunzi kwani bwalo la sasa linaonekani ni dogo kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo.
Miongoni mwa Miradi iliyotembelewa na Kamati ya Siasa ya Mkoa ni pamoja na Ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Mabasi cha Ngangamfuni, Dampo la Kisasa, Kiwanda cha kutengeneza Mbolea ya Mboji pamoja na ujenzi wa Majengo ya wagonjwa wan je na Mama na moto zahati ya Njoro kata ya Njoro.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi