Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya mwaka wa fedha 2020/2021 ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na kuridhishwa na utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni Ujenzi wa Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Njoro,Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na Ujenzi wa watundu 5 ya vyoo katika shule ya Msingi Mandela, Ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Karanga,Ujenzi wa Standi Ngangamfuni na ukarabati wa shule kongwe ya Moshi sekondari.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Patrick alisema ni lengo la Ziara hii ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2020/2025 na wajumbe kuona na kuhakikisha ilani hiyo inatekelezwa kwa kujenga miradi ya Maendeleo ambayo imelenga kutatua changamoto za wananchi kwenye sekta za Elimu, Utawala, na usafirishaji.
“Tunamshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Moshi na hii inadhihirisha kuwa CCM tuliahidi mambo na tunateleleza “Alisema Boisafi
Boisafi katika majumuisho ya ziara hiyo, alisema kamati ya Siasa Mkoa wa Kilimanjaro imeridhishwa na kasi ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, na kutoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi Saidi Mtanda na Mstahiki Meya Juma Raibu kwa kusimamia utekeleza Miradi ya maendeleo kwa ufanisi.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi