Halmashauri ya Manispaaa ya Moshi kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imefanikiwa kukusanya mapato ya ndani kiasi shilingi 5,964,356.906 ambazo ni sawa asilimia 96.40 ya lengo lililowekwa la kukusanya kiasi cha shilingi 6,186,836,000 .
Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi wakati akisoma taarifa ya mwaka utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kwa mwaka 2020/2021 wakati wa Baraza la madiwani lilifanyika katika ukumbi wa Manispaa.
Alieleza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imefanikiwa kukusanya mapato haya ya ndani kutokana na kusimamia vizuri matumizi ya mfumo ya Kieletroniki wa LGRCS (The Local Government Revenue Collection Information System ) ambao umerahisisha utuoaji huduma kwani umeunganishwa na watoa huduma wengine kama vile mabenki na kampuni za simu.
“Tulijiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 6.1 lakini kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Corona ulivyoathiri biashara na makampuni mbalimbali hadi kufikia juni 30 2021 tumefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi billion 5.9 sawa na asilimia 96.45” Alisema Mtahili Meya Raibu
Tunawashukuru wale wote waliotoa waliofanikisha ukusanyaji huu wa mapato kwa fedha hizi zimetumika kwenye miradi ya maendeleo, uendeshaji wa ofisi, utoaji wa mikopo ya wanawake,Vijana na Walemavu nakutatua changamoto mbalimbali wakazi wa Manispaa ya Moshi.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi