Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Bi Mwanahamisi A. Munkunda ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro ameutaka Uongozi wa Halmshauri Manispaa ya Moshi kuhakikisha unatoa fedha za Lishe kwa wakati ya kutosha kulingana na bajeti ili kusaidia juhudi katika kuboresha huduma za lishe kwa wananchi na kufanikisha mapambano dhidi ya utapiamlo.
Bi Mwanahamisi ametoa Rai hiyo leo 16 Januari , 2025, wakati akiongoza kikao cha Kawaida cha Mapitio ya Bajeti ya Lishe ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi chenye lengo la kupokea na kupitia utekelezaji wa Bajeti ya Lishe ambapo amesema Manispaa ya Moshi inatakiwa kuhakikisha inatoa fedha za undesheshaji wa shughuli za afua za Lishe zinatolewa kwa wakati kwa kuzingatia vigezo
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi