Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) yaipongeza Halmasauri ya manispaa ya Moshi kwa kufanikiwa kutenga asilimia 60 ya mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ikiwa ni mkakati wa kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kutoa huduma bora kwa wananchi..
Pongezi hizi zimetolewa na Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini, Alhaji Omari Shamba wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Siasa Moshi Mjini ya kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
“Tunaipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa kuweza kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo yenye lengo la kutatua kero za wananchi kwenye sekta ya Afya,Elimu na Utawala bora”Alisema Alhaj Shamba
Tunawataka wananchi na watumishi wa Halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inatunzwa na kulindwa ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kunufaisha wananchi.
Katika ziara hiyo Kamati ya Siasa ilikagua mradi wa ukarabati wa zahanati ya Bondeni, ujenzi wa zahati ya Kata ya Njoro,ujenzi wa maabara ya fizikia shule ya sekondari ya JK Nyerere, ujenzi wa choo cha wanafunzi matundu 10, shule ya msingi Msaranga, ujenzi wa choo shule ya sekondari Korongoni na mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kata ya Soweto.
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi