Baraza la Madiwani la Manispaa ya Moshi kwa kauli moja limepitisha mpango na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2024/2025 kwa jumla ya Tshs 56,504,196,920 ikiwa na ongezeko la Tsh. 4,650,263,295.63 sawa na asilimia 8.2.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi Kidumo, alitangaza bajeti hiyo , wakati akifunga kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili na kuidhinisha mapendekezo ya bajeti na kueleaza kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Shs 9,559,631,420, Matumizi ya kawaida ruzuku ya uendeshaji (OC) ni Shs 991,022,000, Miradi ya Maendeleo ni Shs 10,477,245,000 na kwa upande wa Mishahara inatarajiwa kuwa Shs 35,548,298,000 hivyo kufanya jumla ya Bajeti ya Manispaa ya Moshi kuwa Shs 56,504,196,920.
“Manispaa ya Moshi inahikikisha kuwa inatekeleza ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 na imejipanga kuweka nguvu zake zaidi katika ukusanyaji mapato na kusimamia miradi miradi ya maendeleo ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi na wakazi wa Manispaa ya Moshi”alisema Mhandisi Zuberi
Awali akiwasilisha bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Ufuatilia Bi Monica Sana alisema kuwa uundaji wa bajeti ya Manispaa ya Moshi kwa mwaka wa fedha 2024/2025 umezingatia vipaumbele ya Manispaa ambavyo ni kukamilisha miradi viporo,kuboresha ukusanyaji wa mapato kwa kubuni vyanzo vipya na kuboresha ukusanyaji kwenye vyanzo vya zamani, kuboresha miundo mbinu na huduma za kijamii na kulipa madeni ya wazabuni na watumishi,
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi