HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI
UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA
Leseni ni kibali halali kinachotolewa na mamlaka husika kwa ajili ya kufanya biashara
iliyoombwa kulingana na aina ya biashara ikionyesha eneo linalopaswa kufanyika biashara kwa
mujibu wa Sheria.
AINA YA LESENI ZA BIASHARA
Zipo aina mbili (2) kuu za leseni.
1. Leseni za biashara zinazosimamiwa na sheria No. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho
yake mwaka 2004. Mfano : Leseni za Hoteli, Maduka ya rejareja n.k
2. Leseni za vileo zinazosimamiwa na sheria No 28 ya mwaka 1968 na marekebisho yake
ya 1990.
(C) ILI MFANYABIASHARA APATE LESENI YAFUATAYO NI LAZIMA
YATEKELEZWE ( Kwa kundi la 1)
1. Kila mfanyabishara anatakiwa kuomba leseni kwa kujaza fomu za maombi ya leseni
zinazotolewa na Halmashauri kupitia kitengo cha Biashara kwa gharama ya Tshs. 1000/=
tu
2. Kila mfanyabiashara lazima awe na kibali cha kodi ya mapato (Business Tax Clearance
Certificate (BTCC) na Tax Identification Number (TIN).
3. Kwa biashara zilizosajiliwa Brela mfanyabishara ataambatanisha vyeti vya usajili yaani
Certificate of Registration, Extract from Register na Cerificate of Incorporation (Kwa
Makampuni) Pamoja na Hati ya Makubaliano (Memorundum and Articles of
Association).
(D)WAOMBAJI WAPYA:
Mfanyabiashara atatakiwa kujaza fomu ya maombi na kupitisha sehemu zifuatazo:
Kupitisha kwa Afisa Mtendaji wa Kata husika.
Kupitisha kwa Afisa Ardhi/Mipango Miji (kwa baadhi ya Biashara
Mfano: Uoshaji wa magari (car wash,garage), viwanda, ufyatuaji wa tofali n.k.
Kupitisha kwa Afisa Afya wa Manispaa kwa ajili ya usalama/usafi wa jengo kwa
ujumla. Kwa biashara za Hotel za kawaida, vilabu vya pombe,utengenezaji wa
vyakula.
(E) WAOMBAJI WA ZAMANI:
Waombaji wanaoendeleza/kuhuisha (Renewals)watapeleka maombi yao Ofisi ya
Biashara
Wakionyesha Nakala ya Leseni halisi iliyoisha muda wake.
Wafanyabiashara hao baada ya kukamilisha taratibu za awali watatakiwa kwenda
Ofisi ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kupatiwa Tax Clearance Certtificate.
Mfanyabiashara baada ya kupatiwa Tax Clearance atarudi Ofisi ya Biashara kwa ajili
ya malipo ya Ada ya Leseni ambayo hulipiwa Benki (NMB).
Baada ya malipo kufanyika Mfanyabiashara atarudi tena Ofisi ya Biashara kwa ajili
ya Leseni.
Kwa sasa Leseni zinatolewa baada ya kuingiza taarifa za Mfanyabiashara kwenye
kompyuta.
Baada ya zoezi la uingizaji taarifa za Mfanyabishara kukamilika mfanyabiashara
ataandikiwa Leseni.
Ni vyema kuwahi kulipia kwani siku za kulipia Leseni bila faini ni siku 21tu.
(F) MAKOSA YA LESENI (SHERIA NA. 25 KIFUNGU 17 A-H)
1. Ukiendesha biashara bila Leseni ukibainika umetenda kosa (kifungu 17(A).)
2. Ukiendesha biashara sehemu ambayo haikutajwa kwenye Leseni ukibainika utakuwa
umetenda kosa (kifungu 17(I)(C).
3. Ukishindwa kuiweka Leseni ya biashara mahali pa wazi (Conspicuous Place) kwenye
biashara wakati wote wa biashara utakuwa umetenda kosa.
4. Ukishindwa kuonyesha Leseni unapotakiwa kuionyesha Leseni yako mara itakapohitajika
na mamlaka husika utakuwa umetenda kosa.
5. Kutoa taarifa za uongo wakati wa kuomba Leseni ni kosa.
6. Ukishindwa kuitoa au kuiwakilisha kwa Afisa mhusika Leseni ya biashara kwa wakati
unaotakiwa ni kosa Na. 15.
7. Kusema uongo kwa lengo la kupitishiwa ada isiyo kuwa sahihi ni kosa.
(G) MASHARTI YA KUTUMIA LESENI
Kwamba hutaweka masharti yeyote kwa mnunuzi.
Kwamba utatoa risiti kwa mauzo yoyote.
Kwamba utafuata Sheria ya Leseni ya biashara ya 1972.
Kwamba hutauza huduma ya bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora
vilivyowekwa na vyombo vinavyohusika kisheria.
Kwamba Leseni hii inaweza kunyang’anywa wakati wowote ikiwa itaonekana kwamba
uliipata kwa udanganyifu au umekiuka masharti ya Leseni hii.
KUNDI LA PILI
SHERIA HII INAHUSU UUZAJI WA VILEO VYA KIGENI/KIENYEJI
(Sheria Na. 28 ya Mwaka 1968)
WAOMBAJI WAPYA MAOMBI YAO YAPITISHWE MAENEO YAFUATAYO:
Kata
Ardhi/Mipango Miji
Afya
Polisi
Bodi ya Vileo ya eneo husika ndio mamlaka ya ngazi ya mwisho ya Manispaa ya kuruhusu ni
nani apewe leseni na aruhusiwe kuuza aina gani ya vileo na muda wa kufanya biashara
Baada ya kulipia ada ya maombi ambayo kwa mujibu wa Sheria ni Ths. 2,000/= kwa kila ombi
KALENDA:
Leseni ya vileo huwa ni ya miezi sita yaani kuanzia tarehe 1 April hadi tarehe 30 Septemba kwa
Mwaka husika na kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 30 Machi mwaka unaofuata.
Baada ya kikao cha mwanzo Mamlaka inaweza kujadili na kutolea uamuzi maombi ambayo
hayakupitia kwenye kikao cha mwanzo kwa kulipia ada ya Shs. 8,000/= juu ya ada ya kawaida
ya maombi ambayo ni sh. 2,000/= na hivyo kufanya ada ya maombi kwa wanaoleta maombi nje
ya muda uliopangwa kuwa Tshs. 10,000/=
WAOMBAJI WA ZAMANI:
Waombaji wanaondeleza/kuhuisha watapeleka maombi yao Ofisi ya Biashara
wakionyesha Nakala ya Leseni halisi iliyoisha muda wake.
Wafanyabiashara hao baada ya kukamilisha taratibu za awali watatakiwa kwenda Ofisi
ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kupatiwa Tax Clearance Certificate.
Mfanyabiashara baada ya kupatiwa Tax Clearance atarudi Ofisi ya Biashara kwa ajili
ya malipo ya Ada ya Leseni ambayo hulipiwa Benki(NMB).
Baada ya malipo kufanyika Mfanyabiashara atarudi tena Ofisi ya Biashara kwa ajili ya
Leseni.
Kwa sasa Leseni zinatolewa baada ya kuingiza taarifa za Mfanyabiashara kwenye
kompyuta.
Baada ya zoezi la uingizaji taarifa za Mfanyabishara kukamilika mfanyabiashara
ataandikiwa Leseni.
Ni vyema kuwahi kulipia kwani siku za kulipia Ada ya Leseni bila faini ni siku 14 tu.
AINA YA LESENI:
1. Retailers on Licence – Bar
2. Retailers off Licence - Grocery – Off – Licence
3. Wholesale dealers Licence – Kuuza pombe za kigeni jumla
4. Member Club Licence – Leseni ya klabu ya wanachama
5. Local Liquor Licence – Leseni ya pombe za kienyeji
ADA YA LESENI YA VILEO:
Biashara za Vileo hazikufanyiwa marekebisho yeyote ya ada ya Leseni.
Leseni hizo zitaendelea kulipiwa ada ya Leseni kila baada ya miezi sita kama ifuatavyo:
BAR - TSHS. 40,000.00
GROCERY - TSHS. 30,000.00
CLUBS - TSHS. 20,000.00
WHOLESALE - TSHS. 20,000.00
POMBE ZA KIENYEJI - TSHS. 12,000.00
MAKOSA CHINI YA SHERIA HII:
1. Kuendesha shughuli kabla au baada ya saa zilizoruhusiwa.
2. Kuhudumia wateja ambao ni chini ya umri ulioruhusiwa kisheria (miaka 18)
3. Kutokuiweka Leseni ya Vileo katika eneo husika wakati biashara inafanyika (Serving
point ) kwa mfano: Counter
4. Kuendesha vituo vya kuuzua (Serving points)zaidi ya kimoja kwa Leseni moja kwa
mujibu wa Sheria kila counter inatakiwa kuwa na Leseni yake.
SAA ZINAZOKUBADILIKA KISHERIA KWA WAFANYABIASHARA WA VILEO
KWA KUZINGATIA AINA YA LESENI ILIYOTOLEWA.
1. BAR (RETAILERS ON LICENCE):
(i) Jumatatu hadi Ijumaa:
(a) Saa 6:00 Mchana hadiSsaa 8:00 Mchana.
(b) Saa 12:00 hadi 5:00 Usiku.
(ii) Jumamosi, Jumapili na Siku za Sikukuu:
(a) Saa 5:00 Asubuhi hadi Saa 8:00 Mchana.
(b) Saa 11:00 Jioni hadi Saa 6:00 Usiku.
2. GROCERY AND WHOLESALE (RETAILERS OFF LICENCE &
WHOLESALE):
(i) Jumatatu hadi Ijumaa
(a) Saa 2:00 Asubuhi hadi Saa 1:00 Usiku
(ii) Jumamosi,Jumapili na Siku za Sikukuu:
(a) Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 6:00 Mchana
3. RESTAURANTS AND HOTELS:
(i) Jumatatu hadi Ijumaa
(a) Saa 6:00 Asubuhi hadi Saa 8:00 Mchana
(b) Saa 12:00 Jioni hadi Saa 5:00 Usiku
(ii) Jumamosi,Jumapili na siku za sikukuu:
(a) Saa 5:00 Asubuhi hadi Saa 8:00 Mchana.
(b) Saa 11:00 Jioni hadi Saa 6:00 Usiku.
4. MEMBERS CLUB (KLABU YA WANACHAMA):
Masharti yake kama Bar ila pombe ni mali ya Club na inanywewa na wanachama tu.
(i) Jumatatu hadi Ijumaa
(a) Saa 6:00 Mchana hadi Saa 8:00 Mchana
(b) Saa 12:00 Jioni hadi Saa 5:00 Usiku
(ii) Jumamosi,Jumapili na siku za Sikukuu
(a) Saa 5:00 Asubuhi hadi Saa 8:00 Mchana
(b) Saa 11:00 Jioni hadi Saa 6:00 Usiku
5. POMBE ZA KIENYEJI:
(i) Jumatatu hadi Ijumaa
(a) Saa 6:00 Mchana hadi Saa 8:00 Mchana
(b) Saa 12:00 Jioni hadi Saa 5:00 Usiku
(ii) Jumamosi,Jumapili na Siku za Sikukuu
(a) Saa 5:00 Asubuhi hadi Saa 8:00 Mchana
(b) Saa 11:00 Jioni hadi Saa 6:00 Usiku
UHAMISHO WA LESENI:
Kila Mfanyabiashara atakaye hamisha biashara kutoka eneo moja kwenda eneo jingine
anapaswa kuandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kupitia kwa Afisa Mtendaji wa
kata Biashara inakohamia na gharama za Uhamisho ni Shs Elfu kumi tu 10,000/=
UPOTEVU WA LESENI:
Mfanyabiashara aliyepoteza /kuibiwa Leseni anapaswa kutoa taarifa kituo cha polisi Wilaya ili
apewe kibali cha Upotevu wa Leseni (Loss report). Baada ya kupata kibali cha Upotevu
akipeleke katika Ofisi ya Halmashauri Kitengo cha Biashara na atalipishwa Tshs
20,000/=kwa ajili ya kupata Nakala ya Leseni.
KUFUNGA BIASHARA:
Kila Mfanyabiashara atakayesimamisha/kuacha kufanya biashara atapaswa kuandika barua kwa
Mkurugenzi wa Manispaa kupitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata husika.
NB:
Pamoja na taratibu zilizoanishwa hapo juu Mfanyabiasha anapaswa kulipia Ada zifuatazo:
1. Ushuru wa Huduma (Service Levy)
2. Ada ya Mabango (Billboard Fee)
3. Hotel Levy kwa Biashara za Hotels,Guest house na Lodge (Hulipwa kila Mwezi)
4. Ada ya Ukaguzi wa Jengo la Biashara (Inspection Fee for Business premise)
5. Ada ya Uzoaji taka(Refuse Collection Fee)
6. Ada ya Upimaji Afya kwa wahudumu wa nyumba za kulala wageni na wauzaji
vyakula.(Medical Examination F
MOSHI MANISPAA KILIMANJARO
Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI
Simu: +255-027-2752906
simu ya Mkononi: +255-027-274371/4
Barua Pepe: md@moshimc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi